Watafiti wa Kiirani wafanikiwa kuainisha sehemu sahihi ya tishu ya saratani
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i116700-watafiti_wa_kiirani_wafanikiwa_kuainisha_sehemu_sahihi_ya_tishu_ya_saratani
Wataalamu wa teknolojia na watafiti wa Iran wamefanikiwa kutengeneza bidhaa inayotambua eneo halisi la uvimbe na kurahisisha kuondoa tishu za saratani.
(last modified 2024-09-23T22:49:28+00:00 )
Sep 23, 2024 22:49 UTC
  • Watafiti wa Kiirani wafanikiwa kuainisha sehemu sahihi ya tishu ya saratani

Wataalamu wa teknolojia na watafiti wa Iran wamefanikiwa kutengeneza bidhaa inayotambua eneo halisi la uvimbe na kurahisisha kuondoa tishu za saratani.

Ugonjwa wa saratani umeenea katika zama hizi, na matibabu ya ugonjwa huu kwa kawaida hufanyika kwa njia ya chemotherapy au upasuaji, lakini wakati mwingine kwa kutumia njia hizi, seli za saratani hupungua au kupotea, na wakati mwingine ukubwa wa uvimbe unakuwa mdogo sana na pia wakati mwingine uvimbe unapungua na kuwa mdogo kiasi kwamba daktari hawezi kuugundua. 

Shirika la habari la Farsi limeripoti kuwa, wataalamu wa teknolojia na watafiti wa Kiirani wamefanikiwa kutengeneza  sindano inayofanana na ndoano ya kuvulia samaki ambayo iitasalia imara katika eneo la tishu za saratani;  na hivyo kuwezesha kuondolewa kwa  urahisi zaidi tishu za saratani.

Kwa mujibu wa ripoti hii, bidhaa hii awali ilikuwa haizalishwi hapa nchini lakini sasa imefikia katika marhala ya kibiashara. Moja ya bidhaa ambayo ilizinduliwa katika mkutano wa 22 wa kila mwaka wa Pardis Technology Park ilikuwa bidhaa hii.

Zahra Abid, Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Teknolojia ya Iran, ambaye amekuwa ikifanya kazi katika sekta hii ya teknolojia kwa muda wa miaka 10, amesema: Bidhaa ya kampuni hii ni sindano inayotumika kuweka alama na kuainisha eneo sahihi lenye saratani katika matiti, ambayo hutumika kutambua kwa usahihi uvimbe wa saratani katika upasuaji wa matiti.

Iran yatengeneza kifaa cha kuianisha sehemu sahihi ya tishu ya saratani

Mbali na Iran, ni kampuni moja tu ya Marekani na Ujerumani inayozalisha bidhaa hii maalumu ya matibabu.