Msemaji wa Jeshi la Iran: Marekani imeingia katika kipindi cha kutengwa kimkakati
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i142210-msemaji_wa_jeshi_la_iran_marekani_imeingia_katika_kipindi_cha_kutengwa_kimkakati
Huku akibainisha kuwa Marekani, kwa mara ya kwanza kabisa tangu Vita vya Pili vya Dunia, imeingia katika hali ya "kutengwa kimkakati," msemaji wa Jeshi la Iran amesisitiza kuwa lengo la Marekani katika kuanzisha vita haramu dhidi ya Iran ni kuharibu ustaarabu wa Kiislamu wa Iran.
(last modified 2026-10-15T12:00:31+00:00 )
Oct 15, 2026 11:49 UTC
  • Msemaji wa Jeshi la Iran: Marekani imeingia katika kipindi cha kutengwa kimkakati

Huku akibainisha kuwa Marekani, kwa mara ya kwanza kabisa tangu Vita vya Pili vya Dunia, imeingia katika hali ya "kutengwa kimkakati," msemaji wa Jeshi la Iran amesisitiza kuwa lengo la Marekani katika kuanzisha vita haramu dhidi ya Iran ni kuharibu ustaarabu wa Kiislamu wa Iran.

Brigedia Jenerali Akrami-Nia, msemaji wa Jeshi la Iran, alisema siku ya Jumatano kuwa tofauti kubwa iliyopo kati ya Jeshi la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na majeshi ya mataifa mengine ni uwepo wa imani ya kidini na hali ya kiroho ndani yake. Amesema, Taasisi ya Masuala ya Kiitikadi na Kisiasa ya Jeshi limekuwa na mchango mkubwa katika kukuza mazingira na mijadala ya kiroho ndani ya jeshi hilo.

Ameashiria uchokozi wa kiuoga uliofanywa na adui dhidi ya Iran kupitia vita vya karibuni, na kusisitiza haja ya kukabiliana na simulizi za uongo zinazotungwa na adui ili kujionyesha kama mshindi, akibainisha kuwa watu mashuhuri katika sekta ya utamaduni katika jamii wana jukumu muhimu kuhusu suala hili.

Msemaji wa Jeshi la Iran ameongeza kuwa: "Watawala wa Marekani walidhani kuwa kwa kumuua Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi ya Kiislamu na makamanda wa kijeshi, wangeweza kuwatia woga watu wa Iran na kuwalazimisha wajisalimishe; lakini watu hao wenye upeo na ushujaa mkubwa, kupitia msimamo wao thabiti wa kihistoria, waliwashangaza maadui na kuvuruga kabisa mipango na njama zao."

Akiashiria matamshi ya upotoshaji wa historia yaliyotolewa hivi karibuni na Marco Rubio, Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Brigedia Jenerali Akrami-Nia amesema: Hotuba ya Rubio, katika eneo la Acropolis nchini Ugiriki, ni mwendelezo wa jitihada za adui huyo za kudhoofisha misingi ya 'nguvu laini'. Amesema matamshi hayo yameondoa barakoa la unafiki na hadaa kutoka kwenye uso wa Marekani na kuanika peupe sura yake halisi inayopinga ustaarabu pamoja na tabia yake ya kiburi na kutaka kutawala wengine. Lengo la watawala wa Marekani katika kuchochea vita vinavyoendelea ni kuharibu ustaarabu wa Kiirani-Kiislamu, na siyo tu kupindua mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.