Mwangwi wa sauti ya makombora ya Iran dhidi ya Israel wasikika duniani kote
Mashambulizi ya makombora ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran dhidi ya utawala ghasibu na wa kigaidi wa Israel yameacha mwangwi mkubwa katika duru za kisiasa, kijeshi na hata baina ya watu wa mataifa, dini na mbari tofauti kote duniani.
Mashambulizi hayo ya aina yake ambayo yamefanyika siku chache tu baada ya mauaji ya kigaidi yaliyofanywa na Israel dhidi ya Sayyid Hassan Nasrullah, aliyekuwa Katibu Mkuu wa Hizbullah, yamefanyika ili kutoa ujumbe kwa ulimwengu mzima kwamba, kambi na Mhimili wa Muqawama hauko peke yake na kwamba Umma wa Kiislamu hautanyamaza kimya kuhusiana na vitendo vya kinyama vya utawala wa Kizayuni wa Israel.
Kwa mara ya kwanza, Iran imetumia makombora ya hypersonic, ambayo ni makombora ya balestiki ya hali ya juu zaidi yaliyotengenezwa na Iran, katika Operesheni Ahadi ya Kweli- 2, na kuthibitisha nguvu na uwezo wake kwa ulimwengu.
Mafanikio ya mashambulizi ya makombora ya Iran yamewafanya watu katika nchi mbalimbali kumiminika mitaani kwa furaha na kuunga mkono Operesheni Ahadi ya Kweli- 2 na kutoa heshima zao kwa Mashahidi Nasrullah, Ismail Haniyeh na wanajihadi wenzao.
Maadhimisho na furaha za watu zilishuhudiwa katika nchi kama Iraq, Bosnia Herzegovina, Iran, Iraq, Palestina inayokaliwa kwa mabavu na kadhalika.

Waziri wa Ulinzi wa Iran anasema, asilimia 90 ya makombora ya Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) ililenga shabaha kwa umakini, lakini vyombo vya habari vya Israel na washirika wake wa Kimagharibi vinaeneza propaganda za kuonyesha kuwa sehemu kubwa ya makombora hayo yametunguliwa. Hata hivyo ukubwa wa mashambulizi hayo na mafanikio yake vimewafanyya Wamagharibi wamefeli katika propaganda hizo. Gazeti la Haaretz la Israel kwenyewe limekiri kwamba makombora ya Iran yamelenga shabaha kwa umakini mkubwa.
Taarifa ya Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) imesisitiza kuwa: Operesheni Ahadi ya Kweli -2 ililenga vituo kadhaa vya anga, kambi za kijeshi na rada, pamoja na vituo vya njama na mipango ya mauaji dhidi ya viongozi wa Muqawama na makamanda wa IRGC.