Pezeshkian: Uhusiano wa Iran na Russia ni wa kimkakati, wenye manufaa makubwa
(last modified Thu, 24 Oct 2024 02:43:32 GMT )
Oct 24, 2024 02:43 UTC
  • Pezeshkian: Uhusiano wa Iran na Russia ni wa kimkakati, wenye manufaa makubwa

Rais Masoud Pezeshkian amesema uhusiano wa Iran na Russia ni "wa kimkakati na wenye manufaa makubwa."

Rais Pezeshkian aliyasema hayo jana Jumatano katika mazungumzo yake na mwenzake wa Russia, Vladimir Putin, kando ya mkutano wa kilele wa BRICS katika mji wa Kazan nchini Russia.

"Ninaamini kuwa uhusiano kati ya Iran na Russia ni wa kimkakati na wenye manufaa makubwa kwa nchi zote mbili," amesema Rais Masoud Pezeshkian na kuongeza kuwa: "Vilevile nauona mfumo wa BRICS, pamoja na Umoja wa Kiuchumi wa Eurasia na Shirika la Ushirikiano la Shanghai kama jukwaa linalofaa kwa mwingiliano mzuri."

Rais Pezeshkian ameeleza matumaini kwamba uhusiano wa kiuchumi, kisiasa, kisayansi, kitamaduni na kibiashara kati ya nchi hizo mbili utapanuka zaidi.

Rais wa Iran pia ameeleza matumaini yake kuwa nchi za BRICS zitaweza kuvunja vikwazo vya Marekani na sera za kiimla za nchi hiyo kwa kufanya kazi pamoja.

Marais Pezeshkian na Putin

Kwa upande wake, Rais wa Russia, Vladimir Putin  amepongeza uhusiano wa karibu kati ya mataifa hayo mawili na kusema, uhusiano huo unaendelea vyema kirafiki na kwa njia ya kujenga.

Rais Putin ameelezea matumaini yake kuwa matokeo ya mashauriano kati ya maafisa wa pande mbili yatarasimishwa hivi karibuni kwa kutiwa saini makubaliano ya kina ya kimkakati.

Tags