Iran: Umoja wa Mataifa umepoteza falsafa ya kuwepo kwake
(last modified Fri, 25 Oct 2024 02:41:14 GMT )
Oct 25, 2024 02:41 UTC
  • Iran: Umoja wa Mataifa umepoteza falsafa ya kuwepo kwake

Msemaji wa Wizara ya Mashauri ya Kiigeni ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, Umoja wa Mataifa umo katika hali ya kupoteza falsafa ya kuwepo kwake.

Ismail Baqaei msemaji wa Wizara ya Mashauri ya Kiigeni ya Iran asema hayo katiika ujumbe wake kwa mnasaba wa Siku ya Umoja wa Mataifa iliyoadhiimishwa jana Alkhamisi. Itakumbukwa kuwa, tarehe 24 Oktoba iliyosadifiana na jana miaka 79 iliyopita, Umoja wa Mataifa ulichukua nafasi ya Jumuiya ya Mataifa.

Wawakilishi wa mataifa yaliyoafikiana katika Vita Vikuu vya Pili vya Dunia, yaani Marekani, Urusi, Uingereza na Ufaransa, waliandaa mazingira ya kuundwa umoja huo; na hatimaye katika mkutano uliofanyika San Francisco, Marekani, wawakilishi kutoka nchi 50 duniani walipitisha sheria za kuundwa umoja huo.

Makao Makuu wa Umoja wa Mataifa-New York

 

Baqaei amekosia viikali utendajii wa Umoja wa Mataifa na kueleza kwamba, taasisi hiyo muhimu imo mbioni kupoteza kabisa faslafa  na malengo ya kuasisiwa kwake.

Msemaji wa Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Iran amesema, Umoja wa Mataifa ulioanzishwa tarehe 24 Oktoba 1945 ili kuokoa vizazi vijavyo kutokana na mateso ya vita na ukatili na kuendeleza utawala wa sheria na haki, sasa umekuwa taasisi isiyo na utendaji na haiwezi kuchukua hatua zozote za pamoja kukomesha mauaji ya kutisha ya halaiki huko Gaza na uuchokozi wa utawala wa Israel ni dhidi ya Lebanon.