IMF yaitahadharisha dunia kuepuka vita vya kibiashara
(last modified Fri, 25 Oct 2024 02:40:46 GMT )
Oct 25, 2024 02:40 UTC
  • IMF yaitahadharisha dunia kuepuka vita vya kibiashara

Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) limeitahadhariisha dunia na kuuiitaka iepuke vita vya kibiashara.

Kwa mujibu wa IMF uchumi wa dunia unaweza kudorora kwa ukubwa wa uchumi wa pamoja wa Ufaransa na Ujerumani, ikiwa kutakuwa na vita vya kibiashara kati ya mataifa makubwa yenye uchumi mkubwa duniani.

Tahadhari hiyo inatolewa wakati wasiwasi ukiongezeka kabla ya uwezekano wa kuchaguliwa tena kwa Donald Trump kuwa Rais wa Marekani katika uchaguzi wa mwezi ujao.

Trump anasema ana mpango wa kuanzisha ushuru wa jumla au ushuru wa hadi 20% kwa bidhaa zote zinazoingia Marekani, wakati Umoja wa Ulaya tayari unapanga kulipiza kisasi ikiwa Washington itaendelea na ushuru huo mpya.

 

Wiki iliyopita, Trump alisema "ushuru ndilo neno zuri zaidi katika kamusi", na mawaziri wa fedha katika soko la kimataifa sasa wanaanza kulichukulia kwa uzito matarajio ya yeye kuanza kutekeleza mawazo hayo.

Naibu Mkurugenzi Mkuu wa IMF Gita Gopinath alisema shirika hilo bado haliwezi kutathmini maelezo mahususi ya mipango ya biashara ya Trump, lakini linafikiria kwamba "ikiwa kuna utenganishaji na utumiaji wa kiwango kikubwa wa ushuru, unaweza kuishia na hasara kwa Pato la Taifa la karibu hadi 7%.

Tags