IRGC: Uhalisia wa kushindwa Israel unakaribia kutimia
(last modified Sat, 09 Nov 2024 03:20:58 GMT )
Nov 09, 2024 03:20 UTC
  • IRGC: Uhalisia wa kushindwa Israel unakaribia kutimia

Kamanda Mkuu wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) amesema kisasi cha hivi karibuni cha Iran dhidi ya Israel kilionyesha sehemu ndogo tu ya uwezo wa taifa hili.

Meja Jenerali Hossein Salami, Kamanda Mkuu wa SEPAH alisema hayo katika mji wa kaskazini mashariki wa Mashhad jana Ijumaa na kuongeza kuwa, "Kushindwa kunakojongea kwa utawala wa Kizayuni kunakaribia kutimia."

Kamanda Salami ameeleza kuwa, Operesheni ya Ahadi ya Kweli ya II sio tu ilionyesha "sehemu kiduchu" ya nguvu kubwa ya makombora ya Iran, lakini pia ilithibitisha kwamba Jamhuri ya Kiislamu inaunga mkono mrengo wa Muqawama hata katika hali ngumu.

Jibu la Iran lilitokana mauaji ya kigaidi ya Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa Harakati ya Mapmabano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas), Ismail Haniyah, Katibu Mkuu wa Hizbullah ya Lebanon, Sayyid Hassan Nasrullah, na kamanda wa IRGC ya Iran, Abbas Nilforoushan.

Makombora ya Iran yakielekea Tel Aviv

Meja Jenerali Salami ameitaja Israel kama moja ya majimbo ya Marekani ambalo linahudumia maslahi muhimu ya Washington katika eneo la Asia Magharibi.

Akibainisha kuwa asilimia 98 ya uchumi wa utawala huo ghasibu umeporomoka, Salami amesema mashambulizi dhidi ya bandari za Israel na ukosefu wa utulivu katik Bahari ya Mediterania yatasababisha kusambaratika kwa utawala huo.