Kiongozi Muadhamu: Tutaendelea kuwa pamoja na wananchi wa Lebanon na Muqawama
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ametoa ujumbe wa maneno kwa ajili ya wananchi na viongozi wa Lebanon walioko kwenye vita hivi sasa na kuwaambia kuwa, sisi hatuna tofauti na nyinyi, tuko pamoja nanyi na tutaendelea kuwa pamoja nanyi.
Ayatullah Sayyid Ali Khamenei ametoa ujumbe huo wa maneno kwa Muqawama wa Lebanon na kusisitiza kwa kusema: "Hatuna tofauti na nyinyi. Tuko pamoja nanyi. Sisi na nyinyi ni kitu kimoja. Machungu yenu ni machungu yetu, mateso yenu ni mateso yetu. Hakuna tofauti baina yenu na sisi, sote ni kitu kimoja."
Ujumbe huo wa Kiongozi Muadhamu umewasilishwa na msoma mashairi ya kidini wa Iran, Meysam Motiee, ambaye ameelekea Lebanon kama sehemu ya kampeni ya kitaifa ya Iran ya kuwafikishia misaada watu wanaodhulumiwa wa Ukanda wa Ghaza na Lebanon.
Motiee ameelekea Lebanon akiandamana na kundi la wanaharakati waliowatemelea wananchi mashujaa wa Lebanon kwa ajili ya kufikisha msaada wa kibinadamu wa Iran.
Shirika la Hilali Nyekundu la Iran limetangaza kuwa limeshapeleka tani 2,200 za msaada kwa wananchi wana Muqawama wa Lebanon.
Tangu mwezi Oktoba 2023, Israel imekuwa ikifanya jinai za kutisha na ukatili wa pande zote dhidi ya wananchi wa Ukanda wa Ghaza na Lebanon ambapo imewafungia njia zote wananchi wa Ghaza na hairuhusu msaada wowote wa maana kuwafikia Wapalestina. Makumi ya maelefu ya Wapalestina na maelfu ya Walebanon wameshauawa shahidi katika jinai hizo za Israel.