Iravani: Iran itaendelea kuwa imara katika kuiunga mkono Syria
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i119708-iravani_iran_itaendelea_kuwa_imara_katika_kuiunga_mkono_syria
Balozi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika Umoja wa Mataifa amezungumzia machafuko ya karibuni ya magaidi huko Syria na kusisitiza kuwa Tehran itaendelea kuiunga mkono Damascus katika kukabiliana na makundi hayo ya kigaidi.
(last modified 2024-12-04T13:05:46+00:00 )
Dec 04, 2024 13:05 UTC
  • Iravani: Iran itaendelea kuwa imara katika kuiunga mkono Syria

Balozi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika Umoja wa Mataifa amezungumzia machafuko ya karibuni ya magaidi huko Syria na kusisitiza kuwa Tehran itaendelea kuiunga mkono Damascus katika kukabiliana na makundi hayo ya kigaidi.

Akizungumza katika kikao cha Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, Amir Saeid Iravani ameashiria wasiwasi wa Tehran kuhusu tatizo la usalama huko Syria na kusema: Iran inatambua haki ya Syria ya kupambana na makundi ya kigaidi kama vile Hay-at Tahrir al-Sham na itaendelea kuwa imara katika kuiunga mkono serikali ya Syria na watu wake katika vita dhidi ya ugaidi.

Wapiganaji wa kundi la kigaidi la Tahrir al Sham 

Balozi Iravani ameongeza kuwa, wakati magaidi walipoushambulia mji wa Aleppo, makundi ya kigaidi yalilishambulia kwa makusudi jengo la ubalozi mdogo wa Iran. Hii ni katika hali ambayo kushambulia majengo ya kidiplomasia na kibalozi ni ukiukaji wa wazi wa sheria za kimataifa; na hakuna mtu, kundi au nchi yenye haki ya kutekeleza vitendo kama hivyo.

Mwakilishi wa Kudumu wa Iran UN amezibebesha dhima nchi kadhaa kufuatia ukiukaji huo wa wazi wa sheria za kimataifa kwa sababu ndizo zinazoyaunga mkono na kuyasaidia makundi hayo ya kigaidi.  

Amir Saeid Iravani amesema: Kiwango na utata wa operesheni za kundi la kigaidi la Tahrir al-Sham na silaha zao za kisasa na ndege zisizo na rubani kunaonyesha namna kundi hilo linavyoungwa mkono na kusaidiwa na nchi ajinabi zikiongozwa na Marekani.