Waandamanaji Tehran walaani mauaji ya kimbari ya Israel yaliyoshadidi Gaza
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i124952-waandamanaji_tehran_walaani_mauaji_ya_kimbari_ya_israel_yaliyoshadidi_gaza
Watu wa Iran wamekusanyika kuonyesha msaada wao wa dhati kwa Wapalestina wanaoteseka kutokana na umwagaji damu wa kikatili na vitendo “visivyo vya kibinadamu” vya utawala wa Israel katika Ukanda wa Gaza ulioko chini ya mzingiro.
(last modified 2025-04-09T09:00:57+00:00 )
Apr 09, 2025 09:00 UTC
  • Waandamanaji Tehran walaani mauaji ya kimbari ya Israel yaliyoshadidi Gaza

Watu wa Iran wamekusanyika kuonyesha msaada wao wa dhati kwa Wapalestina wanaoteseka kutokana na umwagaji damu wa kikatili na vitendo “visivyo vya kibinadamu” vya utawala wa Israel katika Ukanda wa Gaza ulioko chini ya mzingiro.

Waandamanaji walikusanyika katika Uwanja wa Palestina katikati mwa Tehran siku ya Jumatano kulaani vita vya Israel dhidi ya Gaza na ukiukaji wa mara kwa mara wa usitishaji vita ulioanza kutekelezwa katika ardhi ya Palestina mwezi uliopita.

Wakiwa wanapiga kelele za kupinga Israel na Marekani, walionesha chuki kali dhidi ya uhalifu wa Waisraeli na huruma yao kwa watu wa Gaza huku wakibeba picha za viongozi waliouawa wa muungano wa mapambano.

Taarifa iliyotolewa wakati wa maandamano hayo ilisema:
“Tumejikusanya tena leo katika Uwanja wa Palestina mbele ya uhalifu wa utawala wa Kizayuni ili kulaani vitendo visivyo vya kibinadamu vya utawala huu maarufu kwa ukatili wake.”

Taarifa hiyo imebaini kuwa: “mauaji ya maelfu ya wanawake na watoto wasio na hatia, mashambulizi dhidi ya vituo vya afya vinavyosimamiwa na Umoja wa Mataifa, mabomu dhidi ya miundombinu muhimu kama vile mitambo ya kuchuja maji baharini, uharibifu wa urithi wa kihistoria wa mji wa Rafah, kuwekewa mzingiro wa chakula Gaza, kuchomwa kwa makazi ya waandishi wa habari, na maelfu ya uhalifu mwingine ulioibuka kutoka kwa uvimbe wa saratani uitwao Israel katika siku kumi tu zilizopita.”

“Taifa la Iran linatoa wito kwa watu wote huru duniani kuona kwa macho yao ni aina gani ya mhalifu katika historia ameweza kusababisha umwagaji damu wa kiwango hiki na matukio ya kusikitisha kwa muda mfupi wa siku 10 tu?”

Waandamanaji wameeleza jinsi Israel inavyopuuza sheria za kimataifa katika vita vyake vya kikatili dhidi ya Gaza.

“Israel imevifanya vyombo vya kimataifa kama Umoja wa Mataifa, Baraza la Usalama, na Mahakama ya Kimataifa ya Haki kuwa dhaifu, na kuvigeuza kuwa vitu vya kuchezea kwa faida yake.”

Israel imeua zaidi ya Wapalestina 1,390 tangu ilipoanzisha tena kampeni ya mauaji ya kimbari Gaza mnamo Machi 18, baada ya kumaliza kwa upande mmoja usitishaji vita wa miezi miwili uliokuwa umeleta utulivu kiasi katika eneo hilo na kuruhusu kuachiliwa kwa mateka wa Kiyahudi.

Vifo hivyo vimefanya idadi jumla ya waliouawa tangu Oktoba 2023 kufikia 50,752, kwa mujibu wa wizara ya afya ya Gaza. Aghalabu ya waliouawa ni wanawake na watoto.