Araqchi: Ujerumani imeonyesha uadui wake kwa kuunga mkono mashambulizi dhidi ya Iran
(last modified Fri, 04 Jul 2025 03:46:31 GMT )
Jul 04, 2025 03:46 UTC
  • Araqchi: Ujerumani imeonyesha uadui wake kwa kuunga mkono mashambulizi dhidi ya Iran

Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Sayyid Abbas Araqchi amejibu maandishi ya Wizara ya Mambo ya Nje ya Ujerumani katika mtandao wa kijamii wa X kuhusu uamuzi wa Iran wa kusitisha ushirikiano wake na Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki baada ya Israel na Marekani kushambulia vituo vya nyuklia vya Iran.

Awali, akaunti ya mtandao wa X ya Wizara ya Mambo ya Nje ya Ujerumani iliandika kuwa: "Uamuzi wa Iran wa kusimamisha ushirikiano na Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki unatuma ujumbe haribifu: Hatua hii inaondoa uwezekano wowote wa ufuatiliaji wa kimataifa wa mpango wa nyuklia wa Iran, ambao ni muhimu kwa utatuzi wa kidiplomasia. Iran inapaswa kubadilisha uamuzi huo."

Akiashiria ujumbe huo, Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran ameandika kwenye akaunti yake ya X kwamba: Majibu kwa habari ya uwongo: Iran inaendelea kushikamana kwa dhati na Mkataba wa Kuzuia Uenezi na Silaha za Nyuklia (NPT). Kwa mujibu wa sheria mpya iliyopitishwa na Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu (Bunge) katika kukabiliana na mashambulizi haramu ya Israel na Marekani dhidi ya vituo vya nyuklia vya Ira, ushirikiano wa Iran na Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki utaratibiwa kupitia Baraza Kuu la Usalama la Taifa la Jamhuri ya Kiislamu kwa sababu za wazi za kiusalama.

Sayyid Abbas Araqchi ameendelea kusema: Ukweli ni kwamba: Kwa watu wa Iran, kitu kinachotuma "ujumbe haribifu" na kuharibu "suluhisho la kidiplomasia" kiko wazi kabisa: Uungaji mkono wa wazi wa Ujerumani kwa shambulio haramu la Israel dhidi ya Iran, ikiwa ni pamoja na mashambulizi dhidi ya vituo vya nyuklia vinavyolindwa, ambayo yametajwa na Ujerumani kuwa ni "kazi chafu" iliyofanywa Israel kwa niaba ya Magharibi. Kwa jeusi, Ujerumani pia imeunga mkono shambulio haramu la Marekani dhidi ya vituo vya nyuklia vya Iran, ambalo limekiuka sheria za kimataifa, Mkataba wa Kuzuia Uenezaji wa silaha za Nyyukliia na Hati ya Umoja wa Mataifa.

Araghchi ameendelea kuashiria ukiukaji wa wazi wa mapatano ya nyuklia ya JCPOA uliofanywa na Ujerumani kupitia matakwa yake ya kukomeshwa kikamilifu "urutubishaji wa urani" nchini Iran na kuongeza: "Wairani tangu hapo awali, walichukizwa na kulaani uungaji mkono wa kinazi wa serikali ya Ujerumani kwa mauaji ya kimbari yanayofanyika Gaza, na vilevile uungaji mkono wake kwa vita vya Saddam dhidi ya Iran kwa kutoa nyenzo muhimu za kutengeneza silaha za kemikali kwa utawala wa wakati huo wa Iraq."