Wizara ya Ulinzi ya US yanakili droni ya kamikaze ya Iran
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i128512-wizara_ya_ulinzi_ya_us_yanakili_droni_ya_kamikaze_ya_iran
Marekani imenakili na kuzindua toleo lake la ndege ya kivita isiyo na rubani ya Iran ya Shahed-136, katika juhudi za kupanua machaguo ya droni za bei nafuu kwa ajili ya kuzitumia kwneye medani za kisasa za vita.
(last modified 2026-03-17T04:36:21+00:00 )
Jul 19, 2025 10:32 UTC
  • Wizara ya Ulinzi ya US yanakili droni ya kamikaze ya Iran

Marekani imenakili na kuzindua toleo lake la ndege ya kivita isiyo na rubani ya Iran ya Shahed-136, katika juhudi za kupanua machaguo ya droni za bei nafuu kwa ajili ya kuzitumia kwneye medani za kisasa za vita.

Droni hiyo iliyopewa jina la LUCAS, ufupisho wa Mfumo wa Mashambulizi ya Gharama ya Chini usio na Rubani (LUCAS), ndege isiyo na rubani ya Kamikaze ilizinduliwa wakati wa ziara ya Waziri wa Ulinzi wa Marekani, Pete Hegseth Jumatano kwenye maonyesho ya mifumo ya ulinzi huko Pentagon.

Hivi karibuni, Rais Donald Trump wa Marekani alisema ameziomba kampuni za Marekani kutengeneza ndege zisizo na rubani zinazofanana na droni za Iran, ambazo si ghali sana bali zina kasi ya juu na hatari.

Trump alisema, "Niliiambia moja ya kampuni za ulinzi kwamba nahitaji ndege nyingi zisizo na rubani, na unajua, Iran inatengeneza droni nzuri, na wanazitengeneza kwa gharama ya dola 35,000 hadi 40,000." 

Maendeleo makubwa na ya kasi ya Iran katika teknolojia ya ndege zisizo na rubani na uwezo wake wa kufanya mashambulizi ya masafa marefu katika vita vya droni kwa usahihi wa hali ya juu kumeimarisha nguvu za kijeshi za nchi hii katika eneo la Magharibi mwa Asia.

Uzalishaji wa ndege zisizo na rubani za Iran umekuwa miongoni mwa mafanikio ya jeshi la taifa hili katika kutengeneza anuwai ya vifaa vya asili vya kujihami ili kufanya vikosi vya jeshi lake kujitosheleza, mkabala wa vitisho na vikwazo vya miaka mingi vya Wamarekani.

Makamanda wa Iran wannasisitiza kuwa, mchakato wa kutengeneza ndege zisizo na rubani katika Shirika la Utafiti la Jeshi la Ulinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu IRGC unaendelea kwa kasi inayofaa, na kwamba katika siku za usoni, ndege  zingine za kivita zisizo na rubani zitaundwa na shirika hilo.