Khatibzadeh: Uhusiano wa Iran na China mkamilishaji wa mfumo mpya wa kimataifa
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i134264-khatibzadeh_uhusiano_wa_iran_na_china_mkamilishaji_wa_mfumo_mpya_wa_kimataifa
Saeed Khatibzadeh, Naibu Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Iran na Mkuu wa Kituo cha Utafiti wa Kisiasa na Kimataifa ameutaja uhusiano wa Iran na China uliojengeka juu ya msingi wa chaguo la maslahi ya pamoja.
(last modified 2025-12-13T11:41:24+00:00 )
Dec 13, 2025 11:41 UTC
  • Khatibzadeh: Uhusiano wa Iran na China mkamilishaji wa mfumo mpya wa kimataifa

Saeed Khatibzadeh, Naibu Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Iran na Mkuu wa Kituo cha Utafiti wa Kisiasa na Kimataifa ameutaja uhusiano wa Iran na China uliojengeka juu ya msingi wa chaguo la maslahi ya pamoja.

Khatibzadeh amesisitiza kuwa, maingiliano hayo hayatokani na kulazimisha, bali chimbuko lake ni udharura wa kuunda uhusiano wa pande nyingi na wenye mfungamano.

Akigusia mabadiliko ya mazingira ya kimataifa na vikwazo na mashinikizo ya kivita, Khatibzadeh aliutaja uhusiano kati ya nchi hizo mbili kuwa wa kweli, wa kihistoria na wa ustaarabu na kusema: Iran na China zikiwa nguzo mbili muhimu za kusini mwa dunia, zitakwenda kwa kasi na mshikamano zaidi katika kuendeleza maslahi yao ya pamoja na utulivu wa kieneo.

Akihutubia katika kongamano la tatu la majadiliano ya Iran na China Saeed Khatibzadeh: "Baada ya viongozi wa nchi hizo mbili kukubaliana kuboresha uhusiano wa pande mbili hadi kufikia ushirikiano wa kina wa kimkakati  hatimaye Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Jamhuri ya Watu wa China zilitiliana saini hati ya na kuweka hati hii katika hatua ya kivitendo.

Kongamano la tatu la majadiliano ya Iran na China la siku mbili lilliloanza leo hapa mjini Tehran linafanyika kwa hima ya Kituo cha Mafunzo ya Kisiasa na Kimataifa cha Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran ambapo pamoja na mambo mengine linajumuisha warsha na majopo maalumu katika nyanja za ushirikiano wa kiuchumi, teknolojia, nishati mbadala, usalama wa chakula.