Araqchi: Kushambulia maghala ya mafuta ni kuangamiza mazingira
Mar 16, 2026 10:28 UTC
-
Abbas Araqchi
Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amesema kuwa kitendo cha kushambulia maghala ya kuhifadhia mafuta katika mji wa Tehran ni sawa na kuangamiza mazingira.
Abbas Araqchi ametuma ujumbe katika ukurasa wake wa mtandao wa kijamii na kulaani mashambulizi ya Israel katika maghala ya kuhifadhia mafuta katika mji wa Tehran.
Amesema mashambulizi hayo yamekiuka sheria za kimataifa na kwamba yatasababisha madhara ya muda mrefu kwa afya na usalama wa wakazi wa Tehran.
Ameongeza kuwa: Kuchafuliwa udongo na maji ya chini ya ardhi kunaweza kuwa na madhara makubwa kwa binadamu.
Mwanadiplomasia huyo wa ngazi ya juu wa Iran amesema kuwa Israel inapasa kutiwa adabu kutokana na jinai zake za kivita.
Tags