IRGC yashambulia kampuni ya Kimarekani ya Oracle nchini Imarati
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i137764-irgc_yashambulia_kampuni_ya_kimarekani_ya_oracle_nchini_imarati
Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu limetangaza katika taarifa yake kuwa: Limetoa kipigo kikali kwa Kampuni ya Kimarekani ya Oracle kufuatia mauaji ya kigaidi ya Mkuu wa Baraza la Kistratejia la Uhusiano wa Nje la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na mkewe.
(last modified 2026-04-03T05:24:08+00:00 )
Apr 03, 2026 05:24 UTC
  • IRGC yashambulia kampuni ya Kimarekani ya Oracle nchini Imarati

Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu limetangaza katika taarifa yake kuwa: Limetoa kipigo kikali kwa Kampuni ya Kimarekani ya Oracle kufuatia mauaji ya kigaidi ya Mkuu wa Baraza la Kistratejia la Uhusiano wa Nje la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na mkewe.

Idara ya Uhusiano wa Umma ya IRGC imetoa taarifa na kutangaza kuwa: "Kama tulivyokuwa tumetahadharisha, tunazishambulia kampuni za ujasusi za teknolojia ya habari na akili mnemba (AI) ambazo ni miongoni mwa nguzo muhimu za oparesheni za kigaidi za adui, likiwa ni jibu kwa kuuliwa shakhsia wa Iran. 

Kwa mujibu wa IRGC, kufuatia kusambaratishwa miundombinu ya kompyuta ya  kampuni ya Marekani ya Amazon baada ya mauaji ya Brigedia Jenerali Fat'h-Alizadeh, Naibu Kamanda wa Kikosi cha Nchi Kavu cha Kikosi cha IRGC na Kamanda wa Kitengo Maalumu cha Fatihin cha jeshi la kujitolea la Basij, miundombinu ya kituo cha data na kompyuta ya kampuni ya Kimarekani ya Oracle, yenye makao yake makuu huko Imarati (UAE) pia imepigwa pakubwa baada ya mauaji ya kigaidi ya Kamal Kharrazi, Mkuu wa Baraza la Kistratejia la Uhusiano wa Nje la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na mkewe.

Taarifa ya IRGC imeeleza kuwa: "Ikiwa jinai hizo zitakaririwa na mauaji mengine ya kigaidi yakafanywa, kampuni inayofuata inapaswa kuwa tayari kupokea jibu kali."