Pezeshkian: Hakuna maana kufanya mazungumzo na adui anayefanya mauaji, vikwazo na vitisho
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i141996-pezeshkian_hakuna_maana_kufanya_mazungumzo_na_adui_anayefanya_mauaji_vikwazo_na_vitisho
Rais Masoud Pezeshkian wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesisitiza kuwa, hakuna hata moja kati ya hatua na mienendo ya upande huo dhidi ya Iran inayolingana na sheria za kimataifa.
(last modified 2026-10-06T12:18:40+00:00 )
Oct 06, 2026 12:17 UTC
  • Pezeshkian: Hakuna maana kufanya mazungumzo na adui anayefanya mauaji, vikwazo na vitisho
    Pezeshkian: Hakuna maana kufanya mazungumzo na adui anayefanya mauaji, vikwazo na vitisho

Rais Masoud Pezeshkian wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesisitiza kuwa, hakuna hata moja kati ya hatua na mienendo ya upande huo dhidi ya Iran inayolingana na sheria za kimataifa.

Dakta Pezeshkiana amesema hayo katika mazuungumzo yake hapa mjini Tehran na Ararat Mirzoyan, Waziri wa Mambo ya Nje na Biashara ya Kimataifa wa Armenia na kueleza kwamba, “Hakuna maana ya kufanya mazungumzo na adui ambaye kila siku anafanya mauaji, anaweka vikwazo, anatumia shinikizo na vitisho, huku akikiuka makubaliano. Taifa letu pia halikubali mtazamo wa aina hiyo.”

Rais wa Iran, akizungumzia historia nzuri ya Waarmenia nchini Iran, amesema kuwa Waarmenia wanaoishi nchini Iran wamekuwa wakitambulika siku zote kuwa ni watu wenye sifa njema na waaminifu. Amesema historia hiyo nzuri ni miongoni mwa tunu muhimu na za thamani katika uhusiano kati ya mataifa hayo mawili.

Rais Masoud Pezeshkian amesema, tatizo kubwa kati ya Iran na Marekani ni kwamba kila mara nchi hizo zinapoanza mazungumzo, Iran hukabiliwa na mashambulizi ya kijeshi.

Akizungumza kuhusu matukio ya hivi karibuni katika eneo hilo na hali nyeti iliyopo sasa, Pezeshkian amesema Iran imewahi kushambuliwa mara tatu baada ya mazungumzo na Marekani.

Amesema hali hiyo inaonyesha kuwa Marekani hailengi kutafuta suluhu kupitia mazungumzo, bali inalenga kuuangusha mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

Pezeshkian amesema Iran imekuwa ikikabiliwa na changamoto hizo licha ya kushiriki katika mazungumzo, akisisitiza kuwa matukio hayo yameifanya Tehran kuwa na mashaka kuhusu nia halisi ya Washington katika mchakato wa kidiplomasia.

Rais Pezeshkian amesema Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imethibitisha mara kadhaa kuwa inaendesha shughuli zake za nyuklia kwa uwazi na kwa nia ya dhati na kwa ajili ya malengo ya amani.

Pezeshkian amesema Iran imekuwa nchi inayofanyiwa ukaguzi na ufuatiliaji mkubwa zaidi na Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki, IAEA, kuliko nchi nyingine duniani.

Amesisitiza kuwa, Iran imeendelea kuthibitisha utayari wake wa kushirikiana katika masuala ya nyuklia, huku ikipinga mashinikizo na madai dhidi ya shughuli zake za nyuklia zinazofanyika kwa malengo ya amani.