Oct 04, 2016 08:13 UTC
  • Iran: Ugaidi umezuia kufikiwa Malengo ya Maendeleo Endelevu

Balozi wa Iran katika Umoja wa Mataifa amesema ugaidi na misimamo mikali ya kufurutu ada vimekuwa kizingiti kikuu katika kufikiwa Malengo ya Maendeleo Endelevu SDGs.

Gholam Ali Khoshroo, Balozi na Mwakilishi wa Kudumu wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika Umoja wa Mataifa ameiambia Kamati ya Pili ya Kikao cha 71 cha umoja huo kwamba, Tehran ipo makini na inachukulia kwa uzito suala la kutekelezwa ruwaza ya mwaka 2030 katika viwango vyote.

Iran: Ugaidi umezuia kufikiwa ruwaza ya 2030

Mbali na kukabiliana na ugaidi na misimamo ya kuchupa mipaka, Ali Khoshroo ameitaka jamii ya kimataifa kuyavalia njuga masuala mazito na ya msingi ya kijamii, kama vile kupunguza kiwango cha umaskini, kuhakikisha kuwa kila mmoja anapata huduma za afya, makazi bora ya kuishi na maji safi, rasilimali za nishati-jadidika, kushughulikia kadhia ya mabadiliko ya hali ya hewa, kukabiliana na ukataji wa miti, jambo ambalo kila mtu kwenye jamii anapasa kulitekeleza.

Kadhalika Gholam Ali Khoshroo, Balozi na Mwakilishi wa Kudumu wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika Umoja wa Mataifa ameipa changamoto taasisi husika kuhakikisha kuwa sera zote zinazopasishwa na vyombo vya kimataifa zinatekelezwa ili kufanikiza ruwaza ya 2030 sambamba na Malengo ya Maendeleo Endelevu SDGs. 

Tags