Meja Jenarali Jafari: Taifa la Iran litamdhibiti kila atakayejaribu kulichokoza
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i16894-meja_jenarali_jafari_taifa_la_iran_litamdhibiti_kila_atakayejaribu_kulichokoza
Kamanda Mkuu wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran (SEPAH), Muhammad Ali Jafari amesema kuwa, taifa la Iran limejiweka tayari kwa ajili ya kutoa jibu kali na kumdhibiti adui yoyote yule.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Oct 07, 2016 00:56 UTC
  • Meja Jenarali Jafari: Taifa la Iran litamdhibiti kila atakayejaribu kulichokoza

Kamanda Mkuu wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran (SEPAH), Muhammad Ali Jafari amesema kuwa, taifa la Iran limejiweka tayari kwa ajili ya kutoa jibu kali na kumdhibiti adui yoyote yule.

Kamanda Muhammad Ali Jafari ameongeza kuwa, muqawama unaoshuhudiwa leo dhidi ya uistikbari katika eneo la  Mashariki ya Kati, hususan Lebanon, Palestina, Iraq, Yemen na Syria, ni matunda ya vita vya kujihami kutakatifu vya miaka minane nchini Iran. Amesema kujihami kutakatifu taifa la Iran katika vita hivyo, kumegeuka na kuwa kigezo chema duniani. Meja Jenerali Jafari ameyasema hayo katika maadhimisho ya kuwakumbuka mashahidi 1880 wa mji wa Kohgiluyeh na Boyer-Ahmad  na kuongeza kuwa, damu ya mashahidi wa vita hivyo ndiyo ambayo imepelekea kushuhudiwa usalama na amani kubwa iliyopo nchini Iran hivi sasa. 

Sehemu ya mazoezi ya kijeshi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran

Ameongeza kuwa hivi sasa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imezungukwa na nchi ambazo zina machafuko na ukosefu wa usalama katika hali ambayo Iran inatawaliwa na anga ya amani na kwamba usalama na amani hiyo inatokana na kusimama imara taifa hili na wapiganaji wake ambapo katika vita vya miaka minane ya kujihami kutakatifu. Aidha amesema Iran ya Kiislamu itatoa jibu kali na kumdhibiti adui yeyote yule.