Ayatullah Shirazi: Siasa za leo duniani zimejaa uwongo na unafiki
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i22321-ayatullah_shirazi_siasa_za_leo_duniani_zimejaa_uwongo_na_unafiki
Ayatullah Makarim Shirazi ambaye ni miongoni mwa wanazuoni wakubwa wa kidini nchini Iran amekosoa anga ya kisiasa inayotawala dunia hivi sasa akisisitiza kuwa siasa hizo za kimataifa zimegubikwa na hadaa na unafiki.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Dec 28, 2016 23:10 UTC
  • Ayatullah Shirazi: Siasa za leo duniani zimejaa uwongo na unafiki

Ayatullah Makarim Shirazi ambaye ni miongoni mwa wanazuoni wakubwa wa kidini nchini Iran amekosoa anga ya kisiasa inayotawala dunia hivi sasa akisisitiza kuwa siasa hizo za kimataifa zimegubikwa na hadaa na unafiki.

Mwanachuoni huyo wa Kiislamu wa Iran amesema siku baada ya nyingine watu wanazidi kupoteza imani na siasa hizo za kimataifa za hadaa na zilizojengeka kwenye misingi ya uwongo.

Ayatullah Naser Makarim Shirazi, mmoja wa Marjaa Taqlidi wa mjini Qum nchini Iran amefafanua kuwa, Wamagharibi wamechafua anga ya siasa duniani kutokana na misimamo yao ya kindumakuwili na ya kugongana.

Ayatullah Makarim Shirazi

Msomi huyo mashuhuri wa Kiislamu hapa nchini ametoa mfano hai kuhusiana na kukombolewa kikamilifu mji wa Aleppo (Halab) nchini Syria, ambapo Wamagharibi wanalia 'machozi ya mamba' licha ya kuwa wao ndio wahusika wakuu na wafadhili wa magenge ya kigaidi katika nchi hiyo ya Kiarabu. 

Ayatullah Makarim Shirazi amehoji kuwa, "je, ni nani muhusika mkuu wa mauaji ya watoto wa Aleppo?," huku akieleza kusikitishwa kwake na namna dunia ilivyofumbia macho sera za kukinzana za nchi za Magharibi na 'machozi yao ya mamba'.

Mwanachuoni huyo wa Kiislamu wa mji wa kidini wa Qum hapa nchini ameongeza kuwa, siasa za kimataifa za uwongo na unafiki hazijachukua hatua yoyote madhubuti kuhusiana na kadhia ya Yemen, licha ya Mfuko wa Watoto wa Umoja wa Mataifa UNICEF kutanabahisha kuwa, watoto elfu moja nchini Yemen huuawa kila wiki kutokana na mashambulizi ya anga ya Saudi Arabia, magonjwa na utapiamlo kwa kukosa huduma za matibabu.

Jinai za Saudia nchini Yemen na kimya cha UN