Vikwazo vipya vya Marekani dhidi ya Iran; ishara nyingine ya kutoaminika Marekani
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i24697-vikwazo_vipya_vya_marekani_dhidi_ya_iran_ishara_nyingine_ya_kutoaminika_marekani
Wizara ya Hazina ya Marekani jana ilitoa taarifa inayowajumuisha shakhsia 25 wa kisheria na wasio wa kisheria katika orodha ya vikwazo vya Marekani dhidi ya Iran. Marekani imeiwekea Iran vikwazo hivyo vipya kwa kisingizio cha kufanya majaribio ya makombora.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Feb 04, 2017 13:39 UTC
  • Vikwazo vipya vya Marekani dhidi ya Iran; ishara nyingine ya kutoaminika Marekani

Wizara ya Hazina ya Marekani jana ilitoa taarifa inayowajumuisha shakhsia 25 wa kisheria na wasio wa kisheria katika orodha ya vikwazo vya Marekani dhidi ya Iran. Marekani imeiwekea Iran vikwazo hivyo vipya kwa kisingizio cha kufanya majaribio ya makombora.

Baada ya kushindwa katika njama yake ya kuzusha madai katika kadhia ya nyuklia ya Iran na kutiwa saini makubaliano ya JCPOA, Marekani imeonyesha kuwa haipo tayari kuacha kuchukua hatua za kiuhasama dhidi ya taifa la Iran. Kwa sababu hiyo miamala jumla ya Marekani haijabadilika kivyovyote, bali nchi hiyo imebadilisha mbinu na senario zake tu dhidi ya nchi hii.

Makubaliano ya JCPOA yaliyofikiwa kati ya Iran na kundi la 5+1 

Marekani imechukua hatua hiyo ikifuatilia malengo mawili. La kwanza ni kuendeleza siasa za kutaka Iran ionekane kuwa ni tishio katika eneo la Mashariki ya Kati; huku lengo la pili la Washingtoni likiwa ni kutaka kuizima bila ya kutumia nguvu nafasi isiyopingika ya Iran katika uga wa kieneo na kimataifa. Hata hivyo baadhi ya weledi wa mambo wanaamini kuwa, serikali ya Rais Donald Trump wa Marekani hivi sasa inachunguza namna itakavyoweza kuufanya utekelezaji wa makubaliano ya JCPOA kuwa mgumu zaidi na hivyo kufanikiwa kuvirejesha mezani vipengee muhimu vya makubaliano hayo, badala ya kuyachana moja kwa moja makubaliano ya nyuklia ya Iran. Moja ya machaguo yanayochunguzwa sasa na serikali ya Marekani, ni kuhusu kuuomba Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki (IAEA) utekeleze siasa za misimamo mikali dhidi ya Iran. Hata hivyo kuna  shaka kubwa iwapo Trump ataweza kuzishawishi nchi nyingine kumuunga mkono katika mchezo huu mpya wa serikali yake. 

Rais wa Marekani Donald Trump anayeendeleza uhasama dhidi ya Iran

Kwa hivi sasa, baada ya kuingia madarakani serikali ya Trump hali ya mambo huko Washington ni tete na ni wazi kuwa ni vigumu kutabiri kwa usahihi kuhusu hatua mpya ya Rais wa Marekani. Hasa ikizingatiwa kuwa Trump ameonyesha misimamo inayokinzana kuhusu makubaliano ya nyuklia ya Iran.  Kwani aliwahi kusema kwamba, makubaliano hayo ni hatari na pia kuyazungumzia vibaya. Lakini pia wakati wa kusainiwa mikataba ya kuiuzia Iran ndege za abiria za Airbus baada ya kufikiwa makubaliano ya JCPOA,  Trump aligusia maslahi ya kibiashara kati ya Marekani na Boeing na akaeleza kwa nini nchi za Ulaya na zile za Asia zinataka kuwa na mahusiano ya kibiashara na Iran, lakini Marekani haiwezi. Ukitupia jicho miamala iliyopita ya Marekani utaona kuwa, Rais mstaafu wa nchi hiyo Barack Obama alionyesha wazi katika duru yake ya pili ya urais kwamba licha ya kusainiwa makubaliano ya JCPOA , anafuata siasa za wenzake waliotangulia na kwamba urithi anaomwachia Trump pia ni hatua hizo hizo za huko nyuma. Marekani imekuwa ikitekeleza hatua tata dhidi ya Iran licha ya kwamba ndani ya Ikulu ya Marekani (White House) ilishawahi kubainishwa mara kadhaa kwamba kuendeleza vikwazo dhidi ya Iran kwa muda usiofahamika ni jambo lisilowezekana. Michakato hiyo yote inaonyesha kuwa, kuwepo mvutano kati ya Marekani na Iran kunatokana na  taifa la Iran kuwa la kimapinduzi, kuwa na msimamo wa wazi na kupinga kwake uistikbari na sera za kupenda kujitanua za Marekani. Madhali hali hii bado inaendelea, ni dhahir shahir kuwa kwa mtazamo wa Marekani, Iran ni nchi tishio; na wakati huo huo ndani ya harakati hizo kunashuhudiwa nukta moja muhimu na ya msingi yenye kutoa ibra na funzo ya kwamba haifai kuiamini Marekani.