Jeshi la Iran lasisitiza udharura wa kulindwa lango la Bab El Mandab
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i25077-jeshi_la_iran_lasisitiza_udharura_wa_kulindwa_lango_la_bab_el_mandab
Kamanda wa Jeshi la Majini la Iran amesema kuwa suala linalopewa umuhimu zaidi na jeshi hilo kwa sasa ni kulinda usalama wa Ghuba ya Aden, Bahari Nyekundu na lango bahari la Bab El Mandab.
(last modified 2026-02-21T22:51:18+00:00 )
Feb 13, 2017 04:49 UTC
  • Jeshi la Iran lasisitiza udharura wa kulindwa lango la Bab El Mandab

Kamanda wa Jeshi la Majini la Iran amesema kuwa suala linalopewa umuhimu zaidi na jeshi hilo kwa sasa ni kulinda usalama wa Ghuba ya Aden, Bahari Nyekundu na lango bahari la Bab El Mandab.

Admeri Habibollah Sayari amesema kuwa Jeshi la Majini la Iran hadi sasa limesindikiza na kudhamini usalama wa meli 3800 za kibiashara na zinazobeba mafuta za Iran na nyingine elfu 25 za kigeni katika lango bahari la Bab El Mandab na Ghuba ya Aden.

Admeri Habibollah Sayari ameongeza kuwa, msafara wa meli za kivita za Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kwa mara ya kwanza kabisa umefanikiwa kufika na kuzunguka eneo la Rasi ya Tumaini Jema huko kusini mwa Afrika.

Meli ya Jeshi la Majini la Iran

Kamanda wa Jeshi la Majini la Iran amesema kuwa mwanzoni mwa mwaka ujao wa 2018 jeshi hilo litaandaa mkutano wa makamanda wa majeshi ya majini ya nchi za kandokando ya Bahari ya Hindi na kwamba nchi za Ulaya pia zitashiriki katika mkutano huo kama watazamaji.

Jeshi la Iran limekuwa likifanya doria katika Bahari ya Hindi kwa ajili ya kudhamini usalama wa meli za kimataifa na kukabiliana na makundi ya wahalifu kama maharamia wa Somalia na makundi ya kimataifa ya wafanya magendo ya dawa za kulevya.