Iran yakanusha madai ya kutuma silaha nchini Yemen
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i26086-iran_yakanusha_madai_ya_kutuma_silaha_nchini_yemen
Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imekanusha madai kwamba inatuma silaha nchini Yemen na kusisitiza kuwa madai hayo hayana msingi wowote.
(last modified 2026-08-17T09:53:57+00:00 )
Mar 08, 2017 03:19 UTC
  • Iran yakanusha madai ya kutuma silaha nchini Yemen

Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imekanusha madai kwamba inatuma silaha nchini Yemen na kusisitiza kuwa madai hayo hayana msingi wowote.

Msaidizi maalumu wa Spika wa Bunge la Iran katika masuala ya kimataifa Hossein Amir-Abdollahian ameashiria mashambulizi ya kinyama yanayoendelea kufanywa na Saudi Arabia dhidi ya watu wa Yemen na kusema idadi ya makundi ya kigaidi yaliyoko kusini mwa Yemen inazidi kuongezeka na ni tishio kubwa kwa usalama wa kandaa hii na maji ya kimataifa.

Amir-Abdollahian amesema kwa mujibu wa mtazamo wa Iran, njia pekee ya kutatua mgogoro wa Yemen ni mazungumzo ya kisiasa kati ya makundi mbalimbali na kuheshimu matakwa ya watu wa nchi hiyo.

Amir-Abdollahian

Kuhusu uhusiano wa Tehran na Riyadh, msaidizi maalumu wa Spika wa Bunge la Iran amesema mwenendo wa Saudi Arabia katika eneo la Mashariki ya Kati si mzuri na kwamba Riyadh inapaswa kufanya mabadiliko katika siasa zake za kieneo.

Vilevile amepongeza Mkutano wa Kimataifa wa Kuunga Mkono Mapambano ya Palestina uliofanyika wiki kadhaa zilizopita mjini Tehran na kusema makundi ya mapambano ya ukombozi ya Palestina yamekuwa macho zaidi kuhusu harakati za utawala ghasibu wa Israel.