Siku ya jeshi; dhihirisho la nguvu na uwezo wa kujilinda Iran
Leo tarehe 18 Aprili inasadifiana na Siku ya Jeshi la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran. Leo jeshi la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran limeyatumia maadhimisho haya kuonyesha uwezo wake unaoongezeka kila siku ambao kimsingi ni ngome imara ya kukabiliana na wavamizi.
Jeshi la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran limewaonyesha maadui nguvu na uwezo wa kujilinda na kujihami lilionao na kuyapa habari njema mataifa ya Mashariki ya Kati kwamba, jeshi la Iran lina uwezo wa kulinda amani na usalama wa eneo hili. Katika kipindi cha vita vya kujihami kutakatifu, jeshi la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran lilisimama kidete mbele ya maadui wavamizi na kuwaonyesha wavamizi na wale wote waliokuwa wakiota ndoto ya kuiangamiza Iran kwamba, halitatetereka hata kwa sekunde moja katika kutoa jibu kali dhidi ya wavamizi.
Hii leo pia jeshi la Iran likitegemea tajiriba ya kipindi cha kujihami kutakatifu na kwa kutumia uwezo mkubwa na zana za kiulinzi lilizo nazo ambazo zilionyeshwa wakati wa kukaribia maadhimisho ya Siku ya Jeshi, liko tayari kutetea Iran ya Kiislamu yenye nguvu na ikiwa nguvu yenye kujilinda ambayo iko tayari kumuangamiza adui hata nje ya mipaka yake. Uwezo wa kujilinda jeshi la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika miaka ya hivi karibuni baada ya vita vya kichokozi na vya kulazimishwa vilivyoanzishwa na utawala wa Baath chini ya uongozi wa dikteta Saddam Hussein umepiga hatua kubwa mno huku ukitegemea tu utaalamu na ubunifu wa hapa ndani.
Iran imepiga hatua kubwa mno katika uwanja wa vita vya ardhini, baharini na angani na kufikia kiwango cha kisasa ulimwenguni. Maendeleo hayo ni makubwa kiasi kwamba, Iran imeweza kufikia kiwango cha kujitosheleza katika kutengeneza makombora ya kisasa ya balastiki, tekonolojia ambayo inamilikiwa na nchi chache kabisa duniani.
Sehemu ya mafanikio hayo ilionyeshwa wakati wa kukaribia Siku ya Jeshi ambapo Rais Hassan Rouhani alihudhuria maadhimisho hayo.
Ukweli wa mambo ni kuwa, tajiriba na matukio ya sasa katika eneo la Mashariki ya Kati pamoja na harakati za kivamizi zinazoongezeka za Marekani na NATO katika eneo hili nyeti, ni mambo yanayotilia mkazo wajibu wa kuweko udharura wa kuongezwa maandalizi na utayari wa kukabiliana na vitisho tarajiwa kwa kiwango chochote kile. Kwa hakika Jamhuri ya Kiislamu ya Iran yenyewe ni mhanga wa uvamizi na vita vya kulazimishwa.
Ni kwa kuzingatia uhakika huo ndio maana taifa hili linapaswa kulinda kiwango chake cha kujihami kwa namna ambayo, adui asithubuthu hata kutoa vitisho vya vita. Maandalizi hayo yanapaswa kuwa kwa namna ambayo, itamfanya adui atambue kwamba, endapo ataivamia kijeshi Iran basi hatapata matokeo yoyote ghairi ya kuangamizwa.
Nukta iliyo wazi hapa ni kwamba, katu Jamhuri ya Kiislamu ya Iran haijawahi kuanzisha vita dhidi ya taifa lolote lile na kamwe haitafanya hivyo; lakini haitasita hata kidogo kutoa jibu kali kwa uvamizi dhidi yake.
Tabán kusema hivi hakuna maana ya kutoa vitisho, bali ni katika kusisitizia tu uhakika unaojulikana kwa jina la "uwezo na nguvu ya kujilinda" ambao ulionyeshwa na jeshi la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika gwaride la maadhimisho ya Siku ya Jeshi hapa nchini, na huo kwa hakika ni sehemu ndogo tu ya uwezo wa kiulinzi na kijeshi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.