Rouhani: Serikali itawasaidia waathiriwa wa mafuriko kwa uwezo wake wote
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i27976-rouhani_serikali_itawasaidia_waathiriwa_wa_mafuriko_kwa_uwezo_wake_wote
Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameeleza kuwa serikali inafanya jitihada kwa nguvu zake zote ili kuwasaidia na kutatua matatizo waliyonayo waathirika wa mafuriko ya hivi karibuni hapa nchini.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Apr 19, 2017 03:04 UTC
  • Rouhani: Serikali itawasaidia waathiriwa wa mafuriko kwa uwezo wake wote

Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameeleza kuwa serikali inafanya jitihada kwa nguvu zake zote ili kuwasaidia na kutatua matatizo waliyonayo waathirika wa mafuriko ya hivi karibuni hapa nchini.

Mafuriko yaliyotokea siku za Alhamisi na Ijumaa iliyopita katika maeneo mbalimbali ya mkoa wa Azerbaijan Mashariki mbali na kusababisha maafa na hasara za kifedha katika vijiji vya Azarshahr na Ajab Shir, mafurikio hayo yameuwa watu 42 ambapo hadi sasa miili ya watu 37 imepatikana. 

Baada ya kuwasili hii leo katika mkoa wa Azerbaijan Mashariki huko kaskazini magharibi mwa Iran, Rais Hassan Rouhani wa Iran ametoa mkono wa pole kwa familia za wahanga wa mafuriko hayo ya hivi karibuni mkoani humo na kuongeza kuwa: Serikali ya Iran imechukua hatua nzuri za kuwasaidia wananchi wa mkoa huo ulioathiriwa na mafuriko tangu kuanza kwa tukio hilo la kutisha ambapo serikali imekuwa ikifuatilia hatua zilizochukuliwa kupitia mkuu wa mkoa na kumtuma Waziri wa Nishati katika eneo hilo. 

Mafuriko yaliyouathiri mkoa wa Azerbaijan Mashariki nchini Iran

Rais Rouhani amebainisha kuwa, hatua na  shughuli zote za kuwatatulia matatizo wananchi waliokumbwa na mafuriko pamoja na kuchunguza usambazaji wa misaada inayohitajika na kuwapatia mikopo raia waathirika zitachunguzwa katika safari yake hiyo katika mkoa wa Azerbaijan Mashariki.