Rais Rouhani: Wafanyakazi ni fakhari ya uchumi na wananchi wa Iran
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i28506-rais_rouhani_wafanyakazi_ni_fakhari_ya_uchumi_na_wananchi_wa_iran
Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, wafanyakazi ni fakhari ya uchumi na wananchi wa taifa hili.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
May 01, 2017 09:24 UTC
  • Rais Rouhani: Wafanyakazi ni fakhari ya uchumi na wananchi wa Iran

Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, wafanyakazi ni fakhari ya uchumi na wananchi wa taifa hili.

Rais Hassan Rouhani amesema hayo alipokuwa akihutubia katika Haram ya Imam Khomeini (MA) kwa mnasaba wa Siku ya Wafanyakazi Duniani inayojulikana kama Mei Mosi na kubainisha kwamba, wakati bidhaa za Iran zitakaposafirishwa nje ya nchi, hapana shaka kuwa, wafanyakazi watakuwa wakifanya kazi kwa heshima, izza na ladha zaidi.

Amesema kuwa, hii leo bidhaa nyingi za mazao za Kiirani zimekuwa zikisafirishwa katika nchi za kaskazini, magharibi na mashariki mwa nchi na kwamba, hii leo masoko ya nchi za kaskazini yanapokea bidhaa za Kiirani kwa namna ambayo, bidhaa hizo hazikidhi kilio na mahitaji yao.

Rais Rouhani akihutubia kwa mnasaba wa Siku ya Wafanyakazi Duniani

Rais Rouhani amewapongeza wafanyakazi kwa kazi kubwa wanaoyoifanya ya kuihudumia nchi yao.

Sambamba na sherehe hizo za Mei Mosi, serikali ikiwa na lengo la kuleta ustawi na kuboresha hali ya utoaji huduma za bima na matibabu kwa watu milioni 42 walioko chini ya Shirika la Kudhamini Bima, kumezinduliwa vituo saba vya matibabu katika mikoa saba hapa nchini ya Khozestan, Ilama, Semnan, Mazandaran, Azerbaijan ya Magharibi, Kerman na Kordestan. 

Aidha kwa mnasaba wa Siku ya Wafanyakazi Duniani, wafanyakazi 15 bora  na wa kupigiwa mfano katika sekta ya kazi na uzalishaji wametunzwa na kutunukiwa zawadi.