IRGC: Uwezo Jeshi la Iran ni kwa ajili ya amani, usalama
Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran IRGC limesema linalenga kueneza amani katika kanda ya Mashaiki ya Kati na kusisitiza kuwa, uwezo wa kujihami wa Iran ni kwa ajili ya kuimarisha na kujidhaminia usalama.
Hayo yamesema na Kamanda wa IRGC, Meja Jenerali Mohammad-Ali Jafari ambaye ameongeza kuwa, Iran imefanya kwa mafanikio jitihada za kuimarisha usalama wa pamoja katika eneo hili kupitia njia na kuimarisha umoja wa Kiislamu na maslahi ya mataifa ya eneo hilo."
Ameongeza kuwa, "Hii leo adui hana budi ila kukiri kuhusu ustawi wa Iran." Jafari pia amepongeza uwezo mkubwa wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika kanda ya Mashariki ya Kati na kuutaja kuwa 'rasilimali yenye thamani' kwa nchi hii. Aidha amesema IRGC inataka kuwepo amani na kuongeza kuwa, "amani hupatikana na kudumu wakati adui anapokuwa na hofu ya kuanzisha vita dhidi yetu."
Meja Jenerali Jafari amesema IRGC haipendi kujiingiza katika vita wala haipingi maingiliano mazuri na dunia lakini amesema amani haipatikani tu kupitia mazungumzo. "Tunakabiliana na adui ambaye hajui isipokuwa lugha ya vitisho. Kwa hivyo hatuwezi kuzungumza naye kwa lugha asiyoifahamu na tutaraji kupata majibu."
Kamanda wa IRGC pia ameashiria sera haribifu za Saudi Arabia katika eneo la Mashariki ya Kati na uungaji mkono wake kwa makundi ya kigaidi na kusema, ufalme wa Saudi sasa unaekelea kuwa kama 'nchi ya ugaidi wa kiserikali katika kanda hii."