Ayat. Kermani: Marekani imezowea kutenda jinai na kuunga mkono wauaji duniani
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i31770-ayat._kermani_marekani_imezowea_kutenda_jinai_na_kuunga_mkono_wauaji_duniani
Khatibu wa Sala ya Ijumaa iliyosaliwa leo hapa mjini Tehran amesema kuwa, Marekani imezowea kufanya jinai na kuunga mkono makundi yanayomwaga damu za watu na wauaji wakubwa duniani.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jul 14, 2017 10:24 UTC
  • Ayat. Kermani: Marekani imezowea kutenda jinai na kuunga mkono wauaji duniani

Khatibu wa Sala ya Ijumaa iliyosaliwa leo hapa mjini Tehran amesema kuwa, Marekani imezowea kufanya jinai na kuunga mkono makundi yanayomwaga damu za watu na wauaji wakubwa duniani.

Ayatullah Muhammad Ali Muvahhedi Kermani amesema hayo katika hotuba ya Sala ya Ijumaa iliyoswaliwa leo hapa Tehran na sambamba na kuashiria ushindi wa kukombolewa mji wa Mosul na jeshi la serikali ya Iraq kwa kushirikiana na harakati ya wananchi ya Hashdu ash-Sha'abi amesema kuwa, ujumbe wa kukombolewa mji huo ni kwamba, wakati wowote wananchi wanaposimama imara kukabiliana na dhulma, Mwenyezi Mungu huwa anawasaidia.

Jinai zilizokuwa zikifanywa na magaidi wa Daesh walipokuwa wanaudhibiti mji wa Mosul, Iraq

Sambamba na kuashiria namna maelfu ya magaidi kutoka nchi 86 za dunia walivyojiunga na makundi hatari ya kigaidi hususan Daesh na kufanya jinai kubwa huko Syria na Iraq, Khatibu wa Sala ya Ijumaa ya mjini Tehran amefafanua kuwa uungaji mkono wa Marekani na utawala haramu wa Kizayuni wa Israel kwa makundi ya kigaidi, limekuwa ni jambo lililozoeleka. Kadhalika ameashiria uwezo mkubwa wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran SEPAH na kusema kuwa, viongozi wa Marekani wanakiri uwezo mkubwa wa vikosi vya ulinzi vya Iran ambavyo vinamiliki silaha za kisasa kabisa za kiulinzi, kama ambavyo pia Marekani na washirika wake wanatambua vyema kwamba, Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran SEPAH lilishambulia kwa umahiri mkubwa ngome za kundi la Daesh (ISIS) katika eneo la Deir Ezzor nchini Syria kutokea hapa hapa Iran. 

Jeshi la Iraq mjini Mosul

Ayatullah Muhammad Ali Muvahhedi Kermani amesema kuwa, hivi sasa uwezo mkubwa wa jeshi la Iran ni changamoto kubwa kwa Marekani na washirika wake katika eneo la Mashariki ya Kati hususan utawala haramu wa Israel. Kadhalika amezungumzia hatua za kiusahama za Marekani dhidi ya Iran ya Kiislamu ikiwemo vikwazo na mashinikizo ya kiuchumi na kusema kuwa, raia wa Iran wamepambana kwa kiasi kikubwa na mashinikizo hayo ya madola ya Magharibi kwa kipindi cha miongo minne sasa na pamoja na hayo daima wameendelea kushikamana na mfumo wao wa Kiislamu.