Rais Rouhani akataa mwaliko wa kukutana na kufanya mazungumzo na Trump
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i36040-rais_rouhani_akataa_mwaliko_wa_kukutana_na_kufanya_mazungumzo_na_trump
Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran alikataa mwaliko wa kukutana na kufanya mazungumzo na Rais Donald Trump wa Marekani alipokuwa New York kushiriki mkutano wa 72 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa UNGA.
(last modified 2026-03-17T04:36:21+00:00 )
Oct 30, 2017 04:27 UTC
  • Rais Rouhani akataa mwaliko wa kukutana na kufanya mazungumzo na Trump

Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran alikataa mwaliko wa kukutana na kufanya mazungumzo na Rais Donald Trump wa Marekani alipokuwa New York kushiriki mkutano wa 72 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa UNGA.

Hayo yamefichuliwa na Bahram Qassemi, Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran alipofanya kikao na waandishi wa habari hapa mjini Tehran jana Jumapili.

Qassemi amefafanua kuwa: "Mwito wa kufanyika mazungumzo ya pande mbili kati ya Tehran na Washington ulitolewa na Marekani yenyewe, lakini Rais Rouhani hakuukubali."

Mara ya mwisho nchi mbili hizi kufanya mawasiliano ya ngazi ya juu ya moja kwa moja ilikuwa mwaka 2013, wakati ambapo Rais Hassan Rouhani alifanya mazungumzo ya simu na Rais wa wakati huo wa Marekani, Barack Obama. 

Trump akihutubia mkutano wa UNGA

Akihutubia mkutano mkuu wa 72 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa (UNGA) mwezi uliopita wa Septemba, Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya lran alikosoa miamala ya kijahili, michafu, chuki na iliyokosa uelewa na utoaji tuhuma zisizokuwa na msingi wowote ya Rais Donald Trump wa Marekani dhidi ya taifa la Iran.

Aidha aliashiria uvunjaji mikataba wa Marekani katika njia ya utekelezaji wa makubaliano ya nyuklia ya JCPOA na kusema kuwa, uvunjaji huo wa mikataba ya kimataifa unaivunjia heshima na itibari Washington yenyewe.