Jeshi la Majini la Iran lazima shambulizi la maharamia Ghuba ya Aden
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i36837-jeshi_la_majini_la_iran_lazima_shambulizi_la_maharamia_ghuba_ya_aden
Jeshi la Majini la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran limefanikiwa kuzima shambulizi la maharamia dhidi ya meli ya mizigo katika Ghuba ya Aden.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Nov 26, 2017 10:38 UTC
  • Jeshi la Majini la Iran lazima shambulizi la maharamia Ghuba ya Aden

Jeshi la Majini la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran limefanikiwa kuzima shambulizi la maharamia dhidi ya meli ya mizigo katika Ghuba ya Aden.

Manowari za Iran ya Kiislamu za Alvand na Lavan zimeokoa meli ya mizigo ya nchi hii kusini mwa eneo la Ras Sharbitat huko Oman mapema leo asubuhi.

Maharamia wa Ghuba ya Aden wamelazimika kukimbia baada ya kukabiliwa vikali na wanajeshi wa majini wa Iran walipokuwa katika jitahada za kuiteka meli ya mizigo ya Iran iitwayo Caspian Harmony.

Katika fremu ya juhudi za kimataifa za kupambana na uharamia, manowari za Jeshi la Majini la Iran zimekuwa zikilinda doria katika Ghuba ya Aden na Bahari ya Hindi tokea Novemba mwaka 2008.

Maharamia wa Somalia katika Bahari Hindi wakijaribu kuteka meli ya mizigo

Meli hizo za kijeshi za Iran zimesindikiza zaidi ya meli 4,200 za kibiashara katika eneo linalosumbuliwa na maharamia la Ghuba ya Aden tokea mwaka huo 2008, hatua ambayo ilipongezwa na Shirika la Kimataifa la Usafiri wa Majini (IMO).

Jeshi la Majini la Iran limezima mara kadhaa mashambulizi ya maharamia dhidi ya meli za mizigo na mafuta za nchi hii na nchi nyingine katika maji ya kimataifa.