Ayatullah Kermani amuonya Trump juu ya hatua zake chafu dhidi ya Quds
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i38267-ayatullah_kermani_amuonya_trump_juu_ya_hatua_zake_chafu_dhidi_ya_quds
Khatibu wa Swala ya Ijumaa iliyoswaliwa leo Tehran amesema kuwa, maamuzi ya Rais Donald Trump wa Marekani hususan kuutangaza mji wa Quds (Jerusalem) kuwa ni mji mkuu wa utawala wa Kizayuni wa Israel, yatapelekea kusambaratika Marekani yenyewe.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Dec 29, 2017 12:38 UTC
  • Ayatullah Kermani amuonya Trump juu ya hatua zake chafu dhidi ya Quds

Khatibu wa Swala ya Ijumaa iliyoswaliwa leo Tehran amesema kuwa, maamuzi ya Rais Donald Trump wa Marekani hususan kuutangaza mji wa Quds (Jerusalem) kuwa ni mji mkuu wa utawala wa Kizayuni wa Israel, yatapelekea kusambaratika Marekani yenyewe.

Ayatullah Mohammad Ali Muvahhedi Kermani ameyasema hayo katika hotuba ya Swala ya Ijumaa ya leo hapa mjini Tehran ambapo sambamba na kuashiri hatua za Trump ya kuutangaza mji wa Quds kuwa mji mkuu wa utawala wa Kizayuni amebainisha kwamba, hivi sasa Trump yuko katika hatua za kuporomoka na kwamba hatua yake hiyo dhidi ya mji huo, mbali na kwamba imesababisha kukosolewa hata na washirika wake, imeufanya Umoja wa Mataifa nao kulalamikia kitendo hicho.

Rais Donald Trump wa Marekani

Kadhalika khatibu wa Swala ya Ijumaa mjini Tehran ameashiria bajeti ya Dola Trilioni saba zilizotengwa na watawala wa Marekani waliotangulia kwa ajili ya eneo la Mashariki ya Kati na kusema kuwa, pamoja na kiwango chote hicho kilichotengwa kwa ajili ya kutoa pigo kwa dini ya Uislamu, ubinadamu, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na wapigania uhuru duniani, Washington imeshindwa kufikia malengo yake.

Jinai za Saudia, Marekani, Israel nk huko nchini Yemen

Ayatullah Mohammad Ali Muvahhedi Kermani amekosoa jinai za Saudia huko nchini Yemen na kuzitaja jinai hizo kuwa maafa ya kibinadamu. Amesema kuwa, licha ya Saudia kujinadi kuwa kitovu cha Uislamu, lakini inamwaga damu za raia wasio na hatia wa Yemen na hivyo ameutaka utawala wa Aal-Saud kukomesha mauaji yake nchini Yemen.