Khatibu wa Sala ya Ijumaa Tehran: Maadui watapata kipigo kikali
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i44036-khatibu_wa_sala_ya_ijumaa_tehran_maadui_watapata_kipigo_kikali
Imamu wa muda wa Sala ya Ijumaa katika mji wa Tehran amesisitiza kuwa vitisho vya Marekani dhidi ya Iran na hatua ya baadhi ya tawala katika eneo za kuwa bega kwa bega na nchi hiyo havisababishi kuyumba kwa aina yoyote nchini Iran kwa sababu iwapo pande hizo zitaanzisha vita zitashindwa na kuangamizwa.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
May 04, 2018 08:56 UTC
  • Khatibu wa Sala ya Ijumaa Tehran: Maadui watapata kipigo kikali

Imamu wa muda wa Sala ya Ijumaa katika mji wa Tehran amesisitiza kuwa vitisho vya Marekani dhidi ya Iran na hatua ya baadhi ya tawala katika eneo za kuwa bega kwa bega na nchi hiyo havisababishi kuyumba kwa aina yoyote nchini Iran kwa sababu iwapo pande hizo zitaanzisha vita zitashindwa na kuangamizwa.

Akizungumza katika hotuba za Sala ya Ijumaa wiki hii hapa Tehran, Ayatullah Muhammad Ali Muvahedi Kermani ameashiria namna Marekani hivi sasa inavyojaribu kuishawishi Ulaya, Saudi Arabia na utawala wa Israel kuwa pamoja nayo dhidi ya Iran na kuongeza kuwa Iran ya Kiislamu ina nguvu na imesimama imara mkabala na ulimwengu wa kiistikbari. 

Ayatullah Muvahedi Kermani

Imamu wa muda wa Sala ya Ijumaa katika mji wa Tehran amezihutubu Marekani na ulimwengu wa kiistikbari kuwa: Iran iko imara, ina nguvu na haiyumbishwi na njozi hizo. Ameongeza kuwa Uislamu uko imara mbele ya Ukafiri na Iran inajifakharishha kuwa chini ya bendera ya Uislamu. Ayatullah Muvahedi Kermani amesisitiza kuwa Marekani na waitifaki wake wanapasa kufahamu kuwa zitakabiliwa na kipigo kikali haijalishi ni kwa kiasi gani zinapambana na kutoa vitisho mkabala na haki.