Sanaa za mikono, Bandar Abbas, Iran + Video
Iran ni nchi yenye utamaduni mkongwe sana. Ni ya watu wa makabila, kaumu, rangi, sura, ustaarabu, tamaduni na mavazi ya kila namna.
Ni nchi yenye vipindi tofauti vya hali ya hewa kwa wakati mmoja. Baadhi ya maeneo yake huweza kuwa katika kipindi cha baridi kali na theluji kunyesha, lakini wakati huo huo baadhi ya maeneo ya Iran huwa katika joto kali la kupindukia, na mengine katika hali nzuri ya hali ya hewa ya kipindi cha machipuo. Iran ni maarufu kwa jina la Nchi ya Miongo Minne.
Hapa tumeweka video inayoonesha sehemu ndogo ya ujamali na ulimbwende wa kimaumbile wa mkoa wa Hormozgan, wa kusini mwa Iran katika upande wa sanaa za mikono. Tukisema mengi tutapunguza utamu wa video yenyewe, tunastahabu kukuachia mwenyewe uone kwa macho yako, kuliko kukurefushia maneno...
By Golnaar Farnudi & Amir Hossein Pouresmaili - 2018