Amoli Larijani: Marekani haiwezi kuficha jinai za utawala wa Kizayuni
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i44810-amoli_larijani_marekani_haiwezi_kuficha_jinai_za_utawala_wa_kizayuni
Mkuu wa Vyombo vya Mahakama nchini Iran amesema kuwa Marekani inahusika na jinai za karibuni za utawala wa Kizayuni na kwamba maafa hayo yametendwa kufuatia baraka za Marekani kwa utawala huo.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
May 21, 2018 23:12 UTC
  • Amoli Larijani: Marekani haiwezi kuficha jinai za utawala wa Kizayuni

Mkuu wa Vyombo vya Mahakama nchini Iran amesema kuwa Marekani inahusika na jinai za karibuni za utawala wa Kizayuni na kwamba maafa hayo yametendwa kufuatia baraka za Marekani kwa utawala huo.

Marekani tarehe nne mwezi huu ilihamisha ubalozi wake kutoka Telv Aviv hadi Baitul Muqaddas. Uamuzi huo umekabiliwa na radiamali na upinzani mkubwa wa Wapalestina na kuibua mapigano kati ya wanajeshi wa Israel na raia wa Palestina. Wapalestina zaidi ya sitini waliuawa shahidi na wengine karibu elfu tatu kujeruhiwa katika hujuma hiyo ya Wazayuni.  

Mapigano yaliyopelekea kuuliwa shahidi Wapalestina zaidi ya sitini huko Ghaza
 

Akizungumza jana katika kikao cha maafisa wa ngazi za juu wa vyombo vya mahakama, Ayatullah Sadiq Amoli Larijani alieleza kuwa wananchi wanaodhulumika wa Palestina ambao wamekuwa wakimbizi na huku wakiendesha mapambano katika muda wa miaka 70 iliyopita wanafahamu vyema kwamba ni lazima waendeleze mapambano dhidi ya utawala wa Kizayuni. Ameongeza kuwa Marekani pia inapasa kufahamu kuwa haiwezi tena kuficha jinai za utawala wa Kizayuni na kukaliwa kwa mabavu ardhi za Palestina na utawala huo ghasibu. 

Mkuu wa Vyombo vya Mahakama nchini Iran ameashiria pia udhaifu na kujidhalilisha baadhi ya serikali za nchi za Kiislamu mbele ya Marekani na utawala wa Kizayuni na kuongeza kuwa pamoja na kuwa kujidhalilisha huko kumepelekea watenda jinai kuthubutu kuanzisha mkakati kwa jina la Mpango wa Karne, lakini nafsi zenye mwamko zinatambua kuwa mahesbu ya Waislamu yako kando na yale ya serikali hizo na ni wazi kuwa wananchi madhulumu wa Palestina ndio watakaoibuka na ushindi wa uhakika.