Hatibu wa Swala ya Ijumaa Tehran: Zama za ubabe wa Marekani zimepita
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i49201-hatibu_wa_swala_ya_ijumaa_tehran_zama_za_ubabe_wa_marekani_zimepita
Hatibu wa Swala ya Ijumaa ya leo mjini Tehran amezungumzia harakati zilizodhidi ya Iran zinazofanywa na Marekani na kusisitiza kuwa, maafisa wa serikali ya Washington akiwemo Rais wa Marekani Donald Trump wanapaswa kuelewa kuwa, zama za ubabe na sera za mabavu zimefika ukingoni na Marekani inachukiwa na kutengwa zaidi duniani siku baada ya siku.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Nov 02, 2018 12:44 UTC
  • Hatibu wa Swala ya Ijumaa Tehran: Zama za ubabe wa Marekani zimepita

Hatibu wa Swala ya Ijumaa ya leo mjini Tehran amezungumzia harakati zilizodhidi ya Iran zinazofanywa na Marekani na kusisitiza kuwa, maafisa wa serikali ya Washington akiwemo Rais wa Marekani Donald Trump wanapaswa kuelewa kuwa, zama za ubabe na sera za mabavu zimefika ukingoni na Marekani inachukiwa na kutengwa zaidi duniani siku baada ya siku.

Ayatullah Mohammad Ali Movahedi-Kermani amesema katika hotuba za Swala ya Ijumaa ya leo mjini Tehran kwamba, ukitoa tawala kadhaa za Mashariki ya Kati, hii leo hakuna nchi inayounga mkono siasa za Marekani. Ameongeza kuwa, hata nchi za Ulaya ambazo ni waitifaki wakuu wa Marekani hazifuati tena siasa za nchi hiyo na zinaanzisha mikakati ya kukabiliana na sera za serikali ya Washington.

Hatibu wa Swala ya Ijumaa ya Tehran amesisitiza kuwa, hatima ya watawala wa Marekani, utawala haramu wa Israel na Saudi Arabia ni maangamio  na kuongeza kuwa, kufichuliwa kwa jinai na mauaji yaliyofanywa na utawala wa kifalme wa Saudi Arabia dhidi ya mwandishi na mkosoaji wa serikali ya nchi hiyo, Jamal Khashoggi kumeweka wazi sura halisi ya utawala huo.

Bin Salman, mtuhumiwa mkuu wa mauaji ya Khashoggi.

Ayatullah Movahedi-Kermani ameashiria pia mashambulizi yanayoendelea kufanywa na Saudi Arabia dhidi ya watu wa Yemen na kusema, mauaji ya utawala wa Aal Saudi na mzingiro wa Saudi Arabia dhidi ya mamilioni ya Wayemeni  vinafanyika kwa msaada wa Marekani.

Hatibu wa Swala ya Ijumaa ya Tehran pia amezungumzia mashambulizi yaliyofanywa na jeshi la Nigeria dhidi ya Waislamu walioshiriki maombolezo ya mjukuu wa Mtume wetu Muhammad (saw) na kuuwa na kujeruhi makumi miongoni mwao na kusema, kuna udharura wa kupatikana njia ya amani ya maelewano.

Vilevile amesema kuwa mahudhurio ya mamilioni ya Waislamu kutoka pembe mbalimbali za dunia katika shughuli ya Arubaini ya kukumbuka mauaji ya Imam Hussein bin Ali (as) huko Karbala yana ujumbe muhimu na kusisitiza kuwa, kupambana na madhalimu na makafiri ni sehemu ya ujumbe wa washiriki katika shughuli hiyo.