Rais wa Iran kushiriki kongamano la OIC mjini Istanbul, Uturuki
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i4969-rais_wa_iran_kushiriki_kongamano_la_oic_mjini_istanbul_uturuki
Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran hii leo anatazamiwa kuelekea mjini Istanbul nchini Uturuki kushiriki Kongamano la 13 la Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu (OIC).
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Apr 13, 2016 03:11 UTC
  • Rais wa Iran kushiriki kongamano la OIC mjini Istanbul, Uturuki

Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran hii leo anatazamiwa kuelekea mjini Istanbul nchini Uturuki kushiriki Kongamano la 13 la Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu (OIC).

Taarifa kutoka Ofisi ya Rais imesema kuwa, Rais Rouhani anatazamiwa kuelekea Uturuki hii leo na kwamba kesho Alkhamisi anatazamiwa kulihutubia kongamano la OIC. Kadhalika Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran anatazamiwa kukutana na kufanya mazungumzo na viongozi wa nchi za Kiislamu pambizoni mwa mkutano huo.

Akizungumza Jumatatu mjini Tehran, Rais Rouhani alieleza matumaini yake kwamba Kongamano la 13 la Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu litatoa kipaumbele kwa masuala ya amani na mshikamano katika ulimwengu wa Kiislamu, sambamba na kujadili ushirikiano wa nchi hizo katika kukabiliana na ugaidi na misimamo ya kufurutu ada.

Kongamano la 13 la OIC lilianza Jumapili iliyopita, ajenda kuu ikiwa ni masuala ya Palestina, mgogoro miongoni mwa nchi wanachama wa OIC na ugaidi.

Kilele cha kongamano hilo kitakuwa kesho Alkhamisi na Ijumaa, ambapo Rais Recep Teyyip Erdogan wa Uturuki atakuwa mwenyeji wa marais na viongozi kutoka nchi zaidi ya 30 za Kiislamu.