Qassemi: Iran ndiyo nchi yenye taathira kubwa zaidi Mashariki ya Kati
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i50561-qassemi_iran_ndiyo_nchi_yenye_taathira_kubwa_zaidi_mashariki_ya_kati
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amesema kuwa, nchi za dunia zimekiri kivitendo kwamba eneo la Mashariki ya Kati haliwezi kushinda na kuondokana na matatizo ya sasa bila ya msaada wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
(last modified 2025-11-07T02:31:33+00:00 )
Jan 01, 2019 14:29 UTC
  • Qassemi: Iran ndiyo nchi yenye taathira kubwa zaidi Mashariki ya Kati

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amesema kuwa, nchi za dunia zimekiri kivitendo kwamba eneo la Mashariki ya Kati haliwezi kushinda na kuondokana na matatizo ya sasa bila ya msaada wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

Bahram Qassemi ameliambia shirika la habari la Mehr kwamba, rekodi ya Iran katika kupambana na ugaidi inaonesha kuwa, Jamhuri ya Kiislamu inataka kudumisha amani na utulivu katika eneo la Mashariki ya Kati na kuzuia machafuko na vita katika eneo hilo. 

Qassemi ameongeza kuwa, daima Iran imekuwa ikisaidia nchi mbalimbali kupambana na ugaidi kadiri ya uwezo wake na kwamba, kwa mujibu wa katiba na mafundisho aali ya Kiislamu, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imekuwa ikifanya jitihada za kuimarisha usalama, kusaidia juhudi za kuwepo ushirikiano wa kikanda na kuwa na uhusiano mwema na nchi zote jirani. 

Bahram Qassemi

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran ameashiria vita vya kinafsi vya Marekani dhidi ya Iran na kusema kuwa, sera za kimsingi za Iran ni kutoingilia masuala ya ndani ya nchi nyingine sambamba na kufanya jitihada za kulinda usalama wa kikanda ambao ni sawa na usalama wake. 

Amesema kuwa Iran haitaruhusu upande wowote kuingilia masuala yake ya ndani na inafanya jitihada za kutengeneza mazingira ya kustawisha uchumi na ushirikiano na nchi nyingine. Amesisitiza kuwa, vita vya kinafsi vya Marekani vinavyotaka kuilazimisha Jamhuri ya Kiislamu ikubaliane na matakwa yasiyo ya haki, vitashindwa na kufeli.