Rais wa Iran: Umoja wa Wapalestina ni njia pekee ya kuishinda Israel
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i50579-rais_wa_iran_umoja_wa_wapalestina_ni_njia_pekee_ya_kuishinda_israel
Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema njia pekee ya taifa madhulumu la Palestina kupata tena haki zake ni kuwa na umoja katika mapambano dhidi ya utawala wa Kizayuni wa Israel.
(last modified 2026-03-27T07:58:19+00:00 )
Jan 02, 2019 04:03 UTC
  • Rais wa Iran: Umoja wa Wapalestina ni njia pekee ya kuishinda Israel

Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema njia pekee ya taifa madhulumu la Palestina kupata tena haki zake ni kuwa na umoja katika mapambano dhidi ya utawala wa Kizayuni wa Israel.

Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameyasema hayo Jumanne mjini Tehran katika mkutano wake na Ziad al-Nakhala, Katibu Mkuu wa Harakati ya Jihad Islami ya Palestina. Rais wa Iran ameashiria miaka 70 ya kusimama kidete taifa la Palestina katika kupambana na uvamizi, dhulma na Wazayuni na kuongeza kuwa: "Waislamu wote wanapaswa kuliunga mkono taifa la Palestina katika kufikia haki zake, kurejea wakimbizi wote wa Palestina, na mji wake mkuu wa daima ukiwa ni Quds Tukufu (Jerusalem).

Rais Rouhani amesisitiza sana kuhusu umoja miongoni mwa Wapalestina na kusema: "Hakuna shaka kuwa, mojawapo ya njia za kufikia ushindi ni umoja wa Wapalestina wote katika mapambano yao dhidi ya utawala wa Kizayuni." Ameendelea kusema kuwa: "Utawala wa Kizayuni ufahamu kuwa, kutokana na muqawama na mapambano ya vijana wa Palestina, hautaweza kuwashinda Wapalestina."

Rais Hassan Rouhani akifanya mazungumzo na ujumbe wa Harakati ya Jihadul Islami ya Palestina

Kwa upande wake Ziad al-Nakhala, Katibu Mkuu wa Harakati ya Jihad Islami ya Palestina amewasilisha ripoti ya matukio ya hivi karibuni katika ardhi za alestina zinazokaliwa kwa mabavu sambamba na utayarifu wa hali ya juu wa makundi ya muqawama na kupigania ukombozi wa Palestina na kusema: "Hakuna shaka kuwa, uungaji mkono na misimamo imara ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imekuwa na nafasi kubwa sana katika kuvunja njama za kufunga failia la kupigania ukombozi wa Palestina.

Aidha amesema, pamoja na kuwepo mashinikizo katika mapambano dhidi ya utawala wa Kizayuni, Wapalestina katika Ukanda wa Ghaza wanaendelea kusimama kidete katika kuvunja njama za mpango wa Marekani unaojulikana kama "Muamala wa Karne". Amesema taifa la Palestina, pamoja na kuwepo mashinikizo na vitisho, litaendeleza mapambano na muqawama.