Njia pekee ya taifa la Iran kukabiliana na adui ni kusimama kidete
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i53459-njia_pekee_ya_taifa_la_iran_kukabiliana_na_adui_ni_kusimama_kidete
Mkuu wa Vyombo vya Mahakama vya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesisitiza kuwa: "Njia pekee ya kukabiliana na shari, fitina, vita vya kiuchumi, kisaikalojia na kisiasa vya adui ni muqawama na kusimama kidete taifa la Iran.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
May 13, 2019 10:55 UTC
  • Njia pekee ya taifa la Iran kukabiliana na adui ni kusimama kidete

Mkuu wa Vyombo vya Mahakama vya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesisitiza kuwa: "Njia pekee ya kukabiliana na shari, fitina, vita vya kiuchumi, kisaikalojia na kisiasa vya adui ni muqawama na kusimama kidete taifa la Iran.

Hujjatul Islam Ibrahimi Raisi, Mkuu wa Vyombo vya Mahakama vya Iran ameyasema hayo leo mjini Tehran katika mkutano na maafisa wa ngazi za juu vya vyombo vya mahakama. Ameongeza kuwa: "Irada ambazo zinafungamana na Mwenyezi Mungu na zenye thamani tukufu zitapata ushindi kwa muqawama na kusimama kidete mbele ya irada za waistikbari na wenye kuleta fitina"

Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu

Mkuu wa Vyombo vya Mahakama vya Iran aidha ameashiria ushindi wa watu wa Ghaza na Yemen wakiwa na mikono mitupu mbele ya tawala za Kizayuni, Saudia na Marekani sambamba na kusambaratisha tawala za kiistikbari na kusema: "Kile ambacho kitapelekea taifa adhimu la Iran lipate ushindi mbele ya hatua hasimu za adui  si mazungumzo na kusalimu amri, bali ni kusimama kidete, mapambano, kumtegemea Mwenyezi Mungu na kujiamini kutokana na uwezo wa kimaada na kimaanawi."