Iran kulinda ardhi yake mbele ya hujuma za adui
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i53898-iran_kulinda_ardhi_yake_mbele_ya_hujuma_za_adui
"Hatutasita hata kidogo katika kulinda ardhi yote na usalama wa taifa wa nchi hii". Haya yamesemwa na Meja Jenerali Mohammad Bagheri Kamanda wa Vikosi vya Majeshi yote ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika ujumbe wake uliotolewa kwa mnasaba wa kutimia mwaka wa 30 tangu mwasisi wa Jamhuri ya Kiislamu hayati Imam Ruhullah Khomeini alipofariki dunia.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jun 03, 2019 21:47 UTC
  • Iran kulinda ardhi yake mbele ya hujuma za adui

"Hatutasita hata kidogo katika kulinda ardhi yote na usalama wa taifa wa nchi hii". Haya yamesemwa na Meja Jenerali Mohammad Bagheri Kamanda wa Vikosi vya Majeshi yote ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika ujumbe wake uliotolewa kwa mnasaba wa kutimia mwaka wa 30 tangu mwasisi wa Jamhuri ya Kiislamu hayati Imam Ruhullah Khomeini alipofariki dunia.

Meja Jenerali Bagheri ameongeza kuwa: Uwezo wa kiulinzi na ushawishi wa kikanda wa Iran ni matokeo ya kuwa hai mfumo na fikra za hayati Imam Khomeini na Kiongozi wa sasa wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Ali Khamenei. Amesema kuwa, taifa la Iran halitasita wala kurudi nyuma katika jitihada zake za kuzidisha uwezo wake wa kujilinda na kuongeza kuwa, Wairani watavifanya vitisho vyote kuwa fursa yenye thamani kubwa kwa ajili ya kustawisha zaidi matunda ya Mapinduzi ya Kiislamu.

Meja Jenerali Bagheri

Kwa hatua zake za kiumajinuni, Marekami inafanya kila iwezalo kulitisha taifa la Iran kupitia bwabwaja za kuanzisha vita dhidi ya Iran. Viongozi wa serikali ya sasa ya Marekani kuanzia Rais wao, Donald Trump, Mshauri wa Usalama wa Taifa John Bolton hadi Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa nchi hiyo Mike Pompeo wanaendeleza mwenendo huo wa kihasama sambamba na kufanya jitihada za kuhalalisha mwenendo huo. Mfano wa mwenendo huo ni matamshi yaliyotolewa Jumapili iliyopita na Mike Pompeo katika mkutano wake na waandishi wa habari mjini Bern akiwa pamoja na mwenyeji wake wa Uswisi, Ignazio Cassis. Pompeo alisema kuwa, Washington iko tayari kufanya mazungumzo na Iran bila ya masharti yoyote lakini wakati huo huo amemesisitiza tena udharura wa kuendelezwa jitihada za Marekani za kile kinatotajwa kuwa ni kutaka kubadilisha mienendo ya Iran.

Pompeo na Ignazio Cassis, Bern

Msemaji wa Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Iran, Sayyid Abbas Mousavi amejibu matamshi hayo ya Pompeo kwa kusema: Tehran haikubali mchezo wa maneno na kueleza malengo ya siri katika kalibu ya maneno mapya. Kigezo kinachopewa umuhimu na Iran ni kuona mabadiliko ya kimsingi katika mienendo ya Marekani kuhusiana na taifa la Iran.

Katika hotuba yake ya hivi karibuni kwenye hadhara ya maafisa wa Mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu kuhusu malengo halisi ya Marekani, Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Ali Khamenei alisema kuwa: Masuala ya kistratijia, kisiasa na kiusalama yana umuhimu sana kwa kila nchi. Masuala haya pia yana umuhimu mkubwa sana kwetu. Wamarekani wanachukizwa na jambo hili na wanataka tufanye biashara nao kuhusu masuala yetu muhimu ya kistratijia, kisiasa na kiusalama; je kuna mtu anayekubali jambo hilo?

Ayatullah Ali Khamenei

Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu alisisitiza kuwa: Kwa msingi huo ni makosa kufanya mazungumzo na Marekani, na kufanya mazungumzo na Wamarekani wasioheshimu chochote ikiwa ni pamoja na maadili, sheria na kanuni za kimataifa ni maskhara na jambo lisilo na maana..

Kuna sababu nyingi zinazoifanya Marekani itake sana kufanya mazungumzo na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran. Hii ni kwa sababu nguvu za Marekani na udhibiti wake duniani unayoyoma na kufifia. Katika upande mwingine Jamhuri ya Kiislamu ya Iran si tu kwamba, haiko katika nafasi dhaifu, bali pia kama alivyosema Kamanda wa Vikosi vya Majeshi ya Jamhuri ya Kiislamu kwa mnasaba wa kumbukumbu ya kuaga dunia hayati Imam Khomeini: Kupanuka kwa stratijia na uwezo wa kikanda wa Iran kumetayarisha mazingira ambayo inakuwa muhali kuweza kutatua jambo lolote katika eneo la Asia magharibi bila ya kuishirikisha Iran.

Meja Jenerali Bagheri

Jamhuri ya Kiislamu kamwe haitaki vita katika eneo hilo lakini dunia inapaswa kuelewa kwamba, mapambano na kusimama kidete katika nyanja zote ndiyo chaguo la taifa la Iran mkabala wa maadui.