Kamalvandi: Iran sasa inarutubisha urani kwa kiwango cha asilimia 4.5
(last modified Wed, 17 Jul 2019 02:37:01 GMT )
Jul 17, 2019 02:37 UTC
  • Kamalvandi: Iran sasa inarutubisha urani kwa kiwango cha asilimia 4.5

Msemaji wa Taasisi ya Nishati ya Nyuklia ya Iran ameeleza kuwa hivi sasa Iran inarutubisha urani kwa kiwango cha asilimia 4.5 (asilimia nne na nusu). Amesema urutubishaji huo ni sawa na treni ya mwendokasi ambapo kituo kitakachofuata kitakuwa ni kutoka asilimia 4.5 hadi 20.

Behruz Kamalvandi jana aliashiria kiwango cha urani ya Iran iliyorutubishwa ambayo imekusanywa na kueleza kuwa: Iran hivi sasa ina kiwango cha urani ya aina hiyo zaidi ya kilo 300 na kwamba kasi ya ukusanyaji pia itaendelezwa. Msemaji wa Taasisi ya Nishati ya Nyuklia ya Iran ameongeza kusema kuwa Iran hivi sasa inahitaji asilimia 4.5 ya urani iliyorutubishwa, na kwamba hata kama kinu cha nyuklia cha Tehran kitahitaji mafuta na Iran kutopatiwa mafuta hayo na nchi za kigeni; nchi hii ina uwezo wa kuyazalisha. 

Msemaji wa Taasisi ya Nishati ya Nyuklia ya Iran amesisitiza namna kiwango cha urutubishaji  hapa nchini kinavyotegemea mantiki ya kiufundi, mahitaji ya nchi na busara ya kisiasa na kusema kuwa: Huenda Iran ikabadili kiwango na asilimia ya urutubishaji wa urani kwa mujibu wa mantiki hiyo ya kisiasa; kama ambavyo ururubishaji umepunguzwa kwa kutegemea mantiki hiyo. 

Behrouz Kamalvandi, Msemaji wa Taasisi ya Nyuklia ya Iran 
 

Tarehe saba mwezi huu Iran ilianza kutekeleza mchakato wa kuvuka kiwango cha  aslimia 3.67 cha urutubishaji wa urani baada ya kumalizika muhula wa siku 60 ilioutoa kwa nchi za Ulaya ili zitekeleze ahadi na majukumu yao kuhusiana na makubaliano ya JCPOA. Iran wakati huo huo imezitahadharisha nchi hizo kwamba Jamhuri ya Kiislamu itachukua hatua ya tatu iliyo kali zaidi iwapo Ulaya itashindwa kutekeleza ahadi zake. 

Tags