Pyongyang kufanyia majaribio ICBM wakati wa uchaguzi wa US?
(last modified Thu, 31 Oct 2024 02:33:45 GMT )
Oct 31, 2024 02:33 UTC
  • Pyongyang kufanyia majaribio ICBM wakati wa uchaguzi wa US?

Korea Kusini imesema yumkini Korea Kaskazini itafanyia majaribio kombora lake jipya la balestiki, lenye uwezo wa kuvuka mabara la ICBM wakati huu wa msimu wa uchaguzi wa rais wa Marekani.

Shirika la habari la Reuters limewanukuu wabunge wa Korea Kusini wakieleza kuwa, Korea Kaskazini kwa mujibu wa taarifa za kijasusi wakisema kuwa, Pyongayang inajiandaa kufanyia majaribio kombora la masafa marefu la ICBM, na huenda ikaamua kulivurumisha wakati wa uchaguzi wa rais wa Marekani.

Jana Jumatano, mbunge wa Korea Kaskazini, Lee Seong-Kwon alisema kitufe cha rununu cha kuvurumisha kombora hilo kimepelekwa katika eneo husika kwa ajili ya jaribio hilo tarajiwa la ICBM na uwezo wake wa kubeba kichwa cha makombora ya nyuklia.

Lee alikuwa akitoa maelezo kwa wanahabari baada ya kikao cha bunge kilichofanyika faraghani, kikiwahohi maafisa wa Shirika la Ujasusi la Ulinzi (DIA). Amesema yumkini jaribio hilo likafanyika kabla, wakati au muda mfupi baada ya uchaguzi rais wa Marekani wa Novemba 5.

Korea Kaskazini ilifanyia majaribio ICBM miaka 7 nyuma

Kombora hilo la kuvuka mabara la ICBM lilifanyiwa majaribio nchini Korea Kaskazini kwa mara ya kwanza miaka saba iliyopita, na kisha jaribio jingine mwaka 2022.

Korea Kaskazini imekuwa ikiendelea kustawisha uwezo wake wa silaha za makombora tangu yalipokwama mazungumzo ya kuishinikiza itokomeze silaha zake za nyuklia na makombora ya balestiki, mkabala wa kupunguziwa vikwazo vilivyolemaza uchumi wa nchi hiyo.

Tags