Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran akutana na mwenzake wa Sweden
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i55496-waziri_wa_mambo_ya_nje_wa_iran_akutana_na_mwenzake_wa_sweden
Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran Muhammad Javad Zarif leo ameendelea na mazungumzo na wakuu wa nchi za Ulaya kwa kukutana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Sweden mjini Stockholm.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Aug 20, 2019 08:55 UTC
  • Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran akutana na mwenzake wa Sweden

Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran Muhammad Javad Zarif leo ameendelea na mazungumzo na wakuu wa nchi za Ulaya kwa kukutana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Sweden mjini Stockholm.

Kwa mjibu wa taarifa, Zarif amekutana na Margot Wallström Waziri wa Mambo ya Nje wa Sweden ambapo wamejadilia maudhi muhimu za kieneo na kimataifa hasa kulinda mapatano ya nyuklia ya Mpango Kamili wa Pamoja wa Utekelezwaji (JCPOA).

Akiwa mjini Stockholm, Zarif pia atakutana na Waziri wa Biashara wa nchi hiyo Anne Linde na Waziri Mkuu wa zamani wa nchi hiyo, Carl Bildt. Halikadhalika Zarif anatazamiwa kukutana na mmiliki wa meli yenye bendera ya Uingereza ambayo inashikiliwa Iran baada ya kukiuka sheria za usafairi wa baharini.

Kesho  Dakta Muhammad Javad Zarif anatazamiwa kukutana na  Waziri Mkuu wa Sweden pamoja na Spika wa bunge la nchi hiyo.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran jana alikuwa nchini Finland ambapo alikutana na viongozi wa nchi hiyo na katika kuendeleza mazungumzo yake na wakuu wa Ulaya ataelekea Norway na kisha Ufaransa.

Mazungumzo ya ujumbe wa kisiasa wa Iran na viongozi wa Finland

Akiwa Helsinki, Zarif alikutana na kufanya mazungumzo  na Rais Sauli Niinisto wa Finland na kujadili masuala ya kieneo na kimataifa. Kujadili masuala ya pande mbili, ushirikiano wa Iran na Ulaya, masuala ya kieneo na kimataifa, kulindwa makubaliano ya nyuklia ya JCPOA na utekelezwaji wa mfumo maalumu wa mabadilishano ya fedha kati ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Umoja wa Ulaya, kwa kifupi INSTEX ni miongoni mwa ajenda kuu za mazungumzo ya Dakta Zarif na viongozi wa Finland.