Rais Rouhani azindua rasmi mfumo wa makombora wa Bavar-373
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i55529-rais_rouhani_azindua_rasmi_mfumo_wa_makombora_wa_bavar_373
Sambamba na maadhimisho ya Siku ya Sekta ya Ulinzi ya Iran tarehe 22 Agosti, Rais Hassan Rouhani leo amezindua rasmi mfumo wa makombora uliotengenezwa na wataalamu wa hapa nchini wenye uwezo wa kupiga shabaha masafa marefu wa Bavar-373.
(last modified 2026-02-21T22:51:18+00:00 )
Aug 22, 2019 02:45 UTC
  • Rais Rouhani azindua rasmi mfumo wa makombora wa Bavar-373

Sambamba na maadhimisho ya Siku ya Sekta ya Ulinzi ya Iran tarehe 22 Agosti, Rais Hassan Rouhani leo amezindua rasmi mfumo wa makombora uliotengenezwa na wataalamu wa hapa nchini wenye uwezo wa kupiga shabaha masafa marefu wa Bavar-373.

Mfumo wa makombora wa Bavar-373 ni miongoni mwa miradi muhimu sana ya makombora ya Iran na uundaji wake ulianza miaka kadhaa iliyopita. Mfumo huo wa makombora una uwezo wa kulenga shabaha hadi umbali wa kilomita 65 angani na kupiga umbali wa karibu kilomita 300 za nchi kavu. 

Mfumo huo wa makombora umebuniwa kwa kuzingatia teknolojia ya kisasa na una uwezo wa kugundua na kutambua malengo 100 kwa wakati mmoja na kupambana na shaba sita kwa wakati mmoja. 

Rais Rouhani akizundua mfumo wa makombora wa Bavar-373

Maafisa wa Wizara ya Ulinzi ya Iran wanasema kuwa, mfumo huo umefanyiwa majaribio yenye mafanikio kwa mara kadhaa. 

Wataalamu wa masuala ya ulinzi wanasema mfumo huo wa makombora wa Bavar-373 wa Iran unafananishwa na S-300 wa Russia na ule wa Patriot wa Marekani na kusisitiza kuwa unazidi mifumo hiyo katika baadhi ya masuala. 

Baada ya kuzinduliwa , Rais Hassan Rouhani ameamuru mfumo huo wa makombora uunganishwe katika mtandao wa ulinzi wa anga wa Iran.