Zarif asisitiza kuhusu udharura wa ushirikiano wa kimataifa
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i56776-zarif_asisitiza_kuhusu_udharura_wa_ushirikiano_wa_kimataifa
Kuweko ushirikiano wa pande kadhaa katika jamii ya kimataifa ni jambo lenye udharura.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Oct 22, 2019 04:26 UTC
  • Zarif asisitiza kuhusu udharura wa ushirikiano wa kimataifa

Kuweko ushirikiano wa pande kadhaa katika jamii ya kimataifa ni jambo lenye udharura.

Suala hilo ndilo lililokuwa ajenda kuu katika hotuba iliyotolewa na Muhammad Javad Zarif Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran kwenye Mkutano wa Kimataifa chini ya anwani "Unilateralism and International Law" hapa Tehran. Suala la udharura wa kuweko ushirikiano wa kimataifa limetiliwa mkazo katika mkutano huo wa Tehran lakini je, ni mambo gani yamepelekea kubadilika mtazamo kuhusu ushirikiano huo katika jamii ya kimataifa; na misimamo ya upande mmoja imekuwa na madhara gani duniani? 

Katika uwanja huo, Zarif amebainisha kuwa serikali kadhaa duniani haziwezi kuchukua maamuzi ya upande mmoja katika masuala ya kimataifa, na kwamba serikali hizo zimefikia natija hii kuwa, zenyewe haziwezi kuyapatia ufumbuzi matatizo ya nchi zao bali haziwezi peke yazo kuzuia hatua za kawaida za nchi nyingine na ndio maana zimeamua kushirikiana katika uwanja huo. 

Washiriki katika Mkutano wa Tehran
 

Katika mazingira ya sasa ambapo matukio yanayojiri duniani yanabainika wazi haraka na taathira zake kuenea kwa kasi katika jamii; matamshi ya Zarif katika mtazamo wa sheria za kimataifa yana umuhimu mkubwa. Jambo hili lilisisitizwa na kuzingatiwa pia katika hotuba ya Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran aliyoitoa katika kikao cha mwaka huu cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa. Rais wa Iran alisema katika kikao hicho kuwa, hatua za upande mmoja si ishara ya nguvu bali ni alama ya udhaifu wa kifikra na kukosa ufahamu kuhusu masuala muhimu na nyeti ya dunia. 

Rais Hassan Rouhani wa Iran katika Mkutano wa Baraza Kuu la UN mjini New York

Sayyid Muhammad Baqir Nourbakhsh mchambuzi a masuala ya kimataifa anatoa tathmini yake kuhusu misimamo kama hiyo katika kalibu ya maamuzi ya pande kadhaa na ya upande mmoja katika uga wa kimataifa kwamba: Sisitizo la Iran juu ya kuimarisha uhusiano kati yake na majirani zake; na kuanzisha mfumo wa pamoja kwa ajili ya eneo la Ghuba ya Uajemi kwa kuzishirikisha nchi zote za eneo hili, kulinda usalama wa Ghuba ya Uajemi na Lango Bahari la Hormoz, kukabiliana na jitihada zozote zenye lengo la kuvuruga usalama katika njia hiyo muhimu ya majini ni nukta ya kuweza kukabiliana na lugha za vitisho na hatua za kupenda vita za Trump.   

Jambo lililo na umuhimu kwa jamii ya kimataifa ni kuheshimu ahadi na makubaliano ya kimataifa, kuaminiana na kufanya mazungumzo. Ni wazi kuwa, matamshi ya Zarif katika mkutano huo wa Tehran yameweka wazi ukweli huu wa mambo. Akiashiaria gharama za kijeshi za Marekani; Zarif amebainisha kuwa: Serikali ya Marekani baada ya matukio ya Septemba 11 ilitumia mabilioni ya dola kwa gharama za kijeshi hata hivyo haikuweza kuwadhaminia usalama raia wake.   

Ishaq Al Habib Balozi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika Umoja wa Mataifa pia alitahadharisha kuhusu suala hili katika kikao cha Jumatatu cha Kamati ya Nne ya Baraza Kuu la umoja huo kwa kusema kwamba: Hatua za fedheha za upande mmoja za serikali ya Marekani katika ngazi ya kimataifa zinaweza kusababisha madhara makubwa kwa amani, usalama na ustawi wa kimataifa.  

Balozi wa Iran UN, Eshaq Al Habib
 

Hata hivyo, tunaweza kukabiliana na hatua hizo za upande mmoja kwa njia gani? Uzoefu wa miaka kadhaa ya karibuni unaonyesha kuwa ushirikiano wa nchi huru unaweza kuzizidishia nguvu nchi hizo za kukabiliana na hatua hizo za upande mmoja. Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imethibitisha kuwa na taathira maamuzi ya pande kadhaa katika kalibu ya tajiriba zake zilizofanikiwa ikiwa ni pamoja na mchango na nafasi yake kuu katika kushughulikia migogoro mbalimbali ya eneo, ikiwemo ya Syria na Iraq. 

Pamoja na hayo, kuna vizuizi na vizingiti mbalimbali katika njia hii. Madola makubwa duniani hayataki kuona nchi nyingine duniani zikichukua maamuzi kuhusu masuala ya kimataifa na  yanayona maslahi yao yakiwa hatarini kuhusu jambo hilo.  Hata hivyo matukio katika eneo yanaonyesha kuwa siasa za pande kadhaa dhidi ya zile za upande mmoja zinaweza kuandaa mazingira mapya mbali na irada ya madola makuu. Kama alivyoeleza Zarif, dunia bila ya ulimwengu wa Magharibi ina maana kuwa, si matukio yote yanajiri katika ulimwengu wa Magharibi na si Magharibi inayoweza kuyatolea maamuzi matukio yote yanayojiri duniani.