Vikwazo na njia za kukabiliana navyo; kwa mtazamo wa Waziri wa Ulinzi
Brigedia Jenerali Amir Hatami Waziri wa Ulinzi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameashiria ukhabithi wa mfumo wa kibeberu dhidi ya Iran ya Kiislamu na kueleza kuwa: Adui hii leo analenga maisha yetu na kujaribu kulisambaratisha taifa hili kwa kutoa pigo kwa Iran ya Kiislamu.
Amir Hatami ameyasema hayo katika kikao cha kitaalamu cha kukabiliana na vikwazo vya kiulinzi dhidi ya Iran. Waziri wa Ulinzi wa Iran ameashiria vikwazo vya mfumo wa ubeberu dhidi ya Iran ya Kiislamu na kueleza kuwa njia pekee ya kukabiliana na vikwazo hivyo ni kuzidisha uwezo na kupanua nguvu katika nyanja zote khususan nguvu ya kiulinzi. Kwa mtazamo wa Waziri wa Ulinzi; vikwazo dhidi ya Iran havitapungua kwa sababu za kina na za msingi. Kwa hiyo njia pekee ya kukabiliana na vikwazo hivyo ni kuzidisha na kupanua uwezo wa nchi nchi hii katika nyanja mbalimbali khususan uwezo wa kiulinzi.
Marekani imetekeleza senario mbili muhimu kuhusu Iran katika miaka miwili iliyopita. Senario ya kwanza: Mashinikizo ya kiwango cha juu zaidi kupitia kubana njia za mahusiano ya kifedha, kibiashara, kibenki, na hata ya kidiplomasia kati ya Iran na nchi za eneo; na pia kuizuia Iran kupata mapato ya mafuta. Senario ya pili ambayo imefuatiliwa kwa wakati mmoja ni utumiaji wa kanali na mirengo ya upashaji habari ili kuzusha maandamano na machafuko na pia kutumia propaganda kwa lengo la kukuza kupita kiasi udhaifu wa serikali.
Sisitizo la Waziri wa Ulinzi wa Iran kuhusu nukta hii kwamba njia pekee ya kukabiliana na vikwazo dhidi ya nchi hii ni kuongeza na kupanua uwezo katika nyanja zote za kimaisha kwa hakika linaashiria njia mbadala ambazo zinapaswa kuchukuliwa katika uwanja huo.
Hakuna shaka kuwa lengo la kushadidishwa vikwazo dhidi ya Iran ni kuiweka nchi hii katika mashinikizo ya kiwango cha juu kabisa. Ndio maana kusimama imara na kukabiliana na mashinikizo hayo ya vikwazo ni jambo gumu na lenye gharama kubwa. Kustahamili vikwazo vya Marekani ambavyo ni ugaidi wa kiuchumi unaotekelezwa na serikali ya Marekani dhidi ya wananchi wa Iran kunategemea mambo mengi. Mbali na kuwa mambo hayo, yanaimarisha miundombinu ya kiuchumi, kunahitajika pia kuwa macho mbele ya mirengo yenye kuvuruga amani na usalama katika jamii. Suala ambalo linapasa kuzingatiwa kwa umakini na hisia kubwa ni nukta hii kwamba Marekani inatumia vikwazo na ugaidi wa kiuchumi kama wenzo wa kuvuruga utulivu wa jamii na kufanikisha malengo yake haramu. Katika mwenendo huo, Marekani inakwamisha waziwazi na kwa uratibu maalumu njia ya kuwadhaminia mahitaji yao wananchi wa Iran kupitia mwenendo wake huo. Bila shaka uchumi na maisha si suala linaloihusu Iran pekee. Huko Marekani pia kutokuwepo usawa katika suala la mapato na ubaguzi; na katika nchi za Ulaya kushindwa serikali za nchi hizo kupunguza nakisi ya bajeti zake yote hayo ni moja ya mambo yanayosababisha matatizo ya kiuchumi na maandamano ya wananchi. Wakati huo huo katika baadhi ya nchi za eneo zilizo tajiri kwa mafuta pia kupungua pakubwa kwa bei ya bidhaa hiyo katika miaka kadhaa ya karibuni kumezidisha matatizo katika mfumo wa uchumi wa nchi hizo; na hivyo kuibua maandamano na ghasia kubwa.
Hakuna shaka kuwa maendeleo na mafanikio ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ni makubwa licha ya nchi hii kukabiliwa na vikwazo vya pande zote. Pamoja na hayo, nchi inapasa kuwa tayari kukabiliana na hali ngumu zaidi. Kwa sababu hiyo, matatizo na masaibu yote ya kiuchumi yanapasa kupatiwa ufumbuzi kupitia jitihada kubwa. Ni wazi kuwa kuwa tayari kukabiliana na vikwazo hivyo vya pande zote dhidi ya Iran yaani vikwazo vya kiulinzi na kiuchumi kunategemea matumizi bora ya suhula zote za ndani kwa kuratibiwa vyema mipango na kuendelea kuwa macho mkabala wa mirengo yenye kuvuruga amani katika jamii. Mbinu zinazotumiwa na vyombo vya habari vya nchi ajinabi katika kuhusu matukio na na matatizo ya kiuchumi ya Iran zinaonyesha wazi kuwa lengo la vyombo hivyo si kukosoa kitaalamu masuala ya kiuchumi bali lengo lao ni kuibua mgogoro wa kisiasa na kutoa pigo kwa mfumo wa utawala nchini hapa.