Hamas yaonya kuhusu kuvunjika kabisa makubaliano ya kusitisha mapigano Gaza
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i141700-hamas_yaonya_kuhusu_kuvunjika_kabisa_makubaliano_ya_kusitisha_mapigano_gaza
Msemaji wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas), huku akisisitiza utayari kamili wa harakati hiyo wa kutekeleza ramani ya njia iliyokubaliwa na ofisi ya Mratibu Maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu mpango wa amani wa Gaza, ameonya kuwa kuvunjika kabisa kwa makubaliano ya kusitisha mapigano na ramani hiyo ya njia kunatokana na utawala unaokalia kwa mabavu ardhi za Palestina kukataa kuheshimu makubaliano hayo.
(last modified 2026-09-25T03:29:31+00:00 )
Sep 25, 2026 03:28 UTC
  • Hamas yaonya kuhusu kuvunjika kabisa makubaliano ya kusitisha mapigano Gaza
    Hamas yaonya kuhusu kuvunjika kabisa makubaliano ya kusitisha mapigano Gaza

Msemaji wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas), huku akisisitiza utayari kamili wa harakati hiyo wa kutekeleza ramani ya njia iliyokubaliwa na ofisi ya Mratibu Maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu mpango wa amani wa Gaza, ameonya kuwa kuvunjika kabisa kwa makubaliano ya kusitisha mapigano na ramani hiyo ya njia kunatokana na utawala unaokalia kwa mabavu ardhi za Palestina kukataa kuheshimu makubaliano hayo.

Hazem Qassem, Msemaji wa Hamas, amesisitiza utayari kamili wa harakati hiyo wa kutekeleza ramani ya njia iliyokubaliwa na ofisi ya Mratibu Maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu mpango wa amani wa Gaza, akibainisha kuwa hatua zote muhimu kwa ajili hiyo zimeshachukuliwa.

Hazem Qassem ameongeza kuwa kuporomoka kabisa kwa makubaliano ya kusitisha mapigano na ramani ya utekelezaji inayohusiana nayo kunatokana na utawala wa Kizayuni kukataa kuzingatia makubaliano hayo na kuongeza mashambulizi dhidi ya wakazi wa Gaza, sambamba na kushindwa kwa Kamati Maalum ya Uratibu na mwakilishi wake, Nickolay Mladenov, kuushinikiza utawala huo kuyatekeleza.

Msemaji huyo wa Hamas amesisitiza umuhimu wa pande zote husika, hasa serikali ya Marekani na Kamati Maalum ya Uratibu, kuwezesha kuingia kwa kamati ya wataalamu katika Ukanda wa Gaza, ili iweze kutimiza majukumu yake kwa wakazi wa eneo hilo na kuanza kupelekwa huko vikosi vya kimataifa kwa mujibu wa makubaliano ya kusitisha mapigano na ramani ya utekelezaji inayohusiana nayo.

Gazeti la Kizayuni la Haaretz awali liliripoti kuwa, kufuatia kukaribia uchaguzi wa utawala wa Kizayuni, mivutano kuhusu hatima ya Ukanda wa Gaza imeongezeka, huku ripoti zikionyesha kuwa watawala wa Israel wanakataa kushirikiana na "Baraza la Amani la Gaza."