Zarif: Kukandamizwa waandamanaji na kukanusha kuchoshwa vibaya Wamarekani kunapaswa kulaaniwa
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i61322-zarif_kukandamizwa_waandamanaji_na_kukanusha_kuchoshwa_vibaya_wamarekani_kunapaswa_kulaaniwa
Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amesema kuwa, mbinu mbovu na za kila siku zinazotumiwa na serikali ya Marekani za ukandamizaji, kuwafunga wapinzani na kukana kuwa Wamarekani wamechoka, ni mambo ambayo yanapaswa kulaaniwa.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
May 31, 2020 03:44 UTC
  • Zarif: Kukandamizwa waandamanaji na kukanusha kuchoshwa vibaya Wamarekani kunapaswa kulaaniwa

Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amesema kuwa, mbinu mbovu na za kila siku zinazotumiwa na serikali ya Marekani za ukandamizaji, kuwafunga wapinzani na kukana kuwa Wamarekani wamechoka, ni mambo ambayo yanapaswa kulaaniwa.

Dk Mohammad Javad Zarif leo Jumapili ametoa tamko rasmi kuhusu machafuko yanayoendelea katika kona zote za Marekani na kusema, serikali ya Marekani inayofanya chokochoko katika mabara ya Asia, Afrika na Amerika ya Latini, inayopenda makuu kupitia kujilimbikizia silaha za kisasa za nyuklia na kuwaunga mkono madikteta wasio na idadi, inafuja vyanzo vya utajiri vya wananchi wake na kuwaongezea mateso wananchi wa Marekani.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amesema, hatupaswi kushangaa tunapoona maandamano yanaendelea nchini Marekani, kwani wananchi wa Marekani wanawataka viongozi wao wawashirikishe katika utajiri wa nchi yao na wawatimizie mahitaji yao.

Ukandamizaji ni mkubwa sana nchini Marekani

 

Amesema, wananchi wa Marekani wamechoshwa na ubaguzi wa rangi, ufisadi, ukosefu wa uadilifu na kutokuwa na hadhi ya kutawala viongozi hao na kwamba dunia inasikia kilio chao.

Jumatatu iliyopita, afisa mmoja mzungu wa jeshi la polisi la mji wa Minneapolis katika jimbo la Minnesota huko Marekani, alimuua kwa damu baridi kabisa raia mmoja mwenye asili ya Afrika kwa kukandamiza goti lake shingoni mwake kwa nguvu zake zote akiwa amemtia pingu mpaka raia huyo anayejulikana kwa jina la George Floyd akakata roho.

Ukatili huo umezusha hasira kubwa nchini Marekani na hadi hivi sasa machafuko yanaendelea. Hata hivyo, Donald Trump amewaita wanaolalamikia ukatili huo kuwa ni magenge ya wahuni na ametishia kuwapiga risasi. Tayari Jeshi la Marekani limetumwa kwenye baadhi ya maeneo ya Marekani kutekeleza amri ya Donald Trump ya kuwapiga risasi waandamanaji.