Iran: Kukandamizwa watu wasio wazungu huko Marekani ni jambo linalousikitisha ulimwengu mzima
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i61347-iran_kukandamizwa_watu_wasio_wazungu_huko_marekani_ni_jambo_linalousikitisha_ulimwengu_mzima
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amesisitiza kuwa, Tehran inapinga uingiliaji wa aina yoyote wa mambo ya ndani ya Marekani lakini ukandamizaji wa kutisha wanaofanyiwa raia wa Marekani hususan wasio wazungu unayaumiza na kuyasikitisha mataifa yoite duniani.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jun 01, 2020 05:27 UTC
  • Iran: Kukandamizwa watu wasio wazungu huko Marekani ni jambo linalousikitisha ulimwengu mzima

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amesisitiza kuwa, Tehran inapinga uingiliaji wa aina yoyote wa mambo ya ndani ya Marekani lakini ukandamizaji wa kutisha wanaofanyiwa raia wa Marekani hususan wasio wazungu unayaumiza na kuyasikitisha mataifa yoite duniani.

Sayyid Abbas Mousavi amesema hayo leo Jumatatu mbele ya waandishi wa habari na huku akigusia madai ya Robert O'Brien, mshauri wa usalama wa taifa wa rais wa Marekani aliyedai kuwa Iran inahusika katika machafuko yanayoendelea hivi sasa nchini Marekani amesema, maandamano na machafuko yanayoshuhudiwa hivi sasa huko Marekani ni matokeo ya miaka mingi ya dhulma na kukandamizwa kupindukia sauti ya wananchi na raia wa Marekani, hivyo viongozi wa Marekani wameshindwa na la kufanya zaidi ya kupayuka na kutoa madai yasiyo na msingi.

Polisi mzungu akimuua Mmarekani Mwafrika Geroge Floyd, kwa damu baridi tena mchana kweupe

 

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amewatumia ujumbe wananchi wa Marekani akisiwaambia, dunia imesikia kilio chenu cha kudhulumiwa na iko pamoja nanyi. Vile vile ameiasa serikali na polisi ya Marekani kwa kusema, acheni kutumia mabavu dhidi ya wananchi wenu, waacheni wapumue.

Aidha ameashiria hatua ya Iran ya kupeleka meli za mafuta nchini Venezuela na kuvunja vikwazo vya Marekani kwa nchi hiyo ya Amerika ya Latini akisema, Iran na Venezuela zimewekewa vikwazo vya kidhulma na Marekani, na hakuna nchi yoyote duniani yenye wajibu wa kuheshimu vikwazo hivyo kama ambavyo pia Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ina msimamo imara wa kulinda haki zake hata katika maeneo ya mbali.

Machafuko yanayoendelea Marekani ni matunda ya ukatili mkubwa nchini humo