Abbas Mousavi: Iran iko tayari kufanya mazungumzo na nchi za Asia Magharibi
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i62316-abbas_mousavi_iran_iko_tayari_kufanya_mazungumzo_na_nchi_za_asia_magharibi
Msemaji wa Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, Tehran iko tayari kufanya mazungumzo na nchi za la Asia Magharibi kwa ajili ya kuyapatia ufumbuzi matatizo mbalimbali yanayolikabili eneo hili.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jul 20, 2020 06:45 UTC
  • Abbas Mousavi: Iran iko tayari kufanya mazungumzo na nchi za Asia Magharibi

Msemaji wa Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, Tehran iko tayari kufanya mazungumzo na nchi za la Asia Magharibi kwa ajili ya kuyapatia ufumbuzi matatizo mbalimbali yanayolikabili eneo hili.

Sayyid Abbas Mousavi sambamba na kubainisha kwamba, daima Iran imekuwa ikifuatilia na kutaka kupatikana amani na uthabiti wa Asia Magharibi na kubainisha kwamba, taifa hili daima limekuwa likiamini suala la kuweko mazungumzo ya kieneo yasiyoingiliwa na madola ya kigeni na inaona kuwa, hiyo ndio njia pekee ya kurejesha amani na hata kuongeza ushirikiano wa kieneo sambamba na kustawisha uchumi wa eneo hili. 

Msemaji wa Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran sambamba na kuashiria kuhusiana na Tehran imetangaza mara chungu nnzima siasa zake za kimsingi na thabiti kuhusiana na Saudi Arabia  na kwamba, inategemea serikali na viongozi wa Riyadh wataamiliana vipi na mitazamo pamoja na mapendekezo ya ushirikiano ya taifa hili

Uchaguzi wa Bunge nchini Syria ulifanyika jana JUmapili 19.07.2020

Msemaji wa Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameashiria pia kufanyika uchaguzi wa Bunge nchini Syria na kueleza kuwa, ana matumaini matokeo ya uchaguzi huo yatakuwa ni hatua moja mbele ya kurejesha amani na utulivu katika nchi hiyo ya Kiarabu.

Ameongeza kuwa, uchaguzi wa Bunge nchini Syria umefanyika kwa mafanikio makubwa katika hali ambayo, waanchi wa nchi hiyo wamevumilia masaibu na machungu mengi yaliyotokana na vita walivyotwishwa, jinai za makundi ya kigaidi, uwepo wa majeshi ya kigeni na vikwazo vya kidhalimu na vya upande mmoja dhidi ya nchi yao.