May 26, 2021 10:41 UTC
  • Rais Rouhani asisitiza kushiriki kwa wingi wananchi katika uchaguzi Iran

Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kufanyika vizuri uchaguzi ni jambo ambalo litadhamini uhalali wa mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

Rais Rouhani ameyasema hayo katika kikao cha baraza la mawaziri ambapo amesema uchaguzi ujao wa rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ni muhimu huku akisisitiza kuhusu kushiriki kwa wingi wananchi katika uchaguzi ujao.

Jana Jumanne, Tume ya Uchaguzi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imetaja majina ya wagombea wa urais katika uchaguzi unaotarajiwa kufanyika mwezi ujao

Katika taarifa yake, tume ya uchaguzi ya Iran imetangaza majina ya wagombea katika uchaguzi wa 13 wa Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran waliotimiza masharti ya kugombea kwa mujibu wa sheria za uchaguzi za Jamhuri ya Kiislamu.

Majina ya wagombea wa uchaguzi wa 13 wa Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran waliotimiza masharti na kupasishwa na Baraza la Kulinda Katiba ni kama ifuatavyo:

Saeed Jalili, Mohsen Rezaee Mirgha'ed, Sayyid Ebrahim Raisol-Sadati (Ebrahim Raisi), Alireza Zakani, Sayyid Amir-Hossein Ghazizadeh Hashemi, Mohsen Mehralizadeh na Abdolnaser Hemmati.

Wagombea urais Iran

Rais Rouhani ambaye anatamiza muhula wake wa pili wa urais haruhusiwi kisheria kugombea mwaka huu.

Uchaguzi wa 13 wa Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na uchaguzi wa 6 wa mabaraza ya Kiislamu ya miji na vijiji unatarajiwa kufanyika Ijumaa ya tarehe  18 mwezi ujao wa Juni, 2021.

Tags